Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kuokoa Ikolojia ya Mto Ruaha kimeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuandaa Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya ardhi ili kuweka ukomo wa matumizi ya ardhi kutambua kila matumizi ya ardhi, elimu ya mazingira ya Halmashauri na jinsi halmashauri iivyojipanga kuhifadhi maji ya mito iliyopo wilayani humo.
Maagizo hayo yametolewa na Kikosi Kazi cha hicho cha Kitaifa wakati wa kukusanya Maoni ya ya Wanasiasa na Watendaji wa Halmashauri ilikupata changamoto na ufumbuzi wake kuhusu kupungua kwa maji katika Mto Ruaha.
Akitoa maagizo hayo Mwenyekiti wa Muda wa Kikosi kazi hicho Mhandisi Seth Luswema amesema kuwa Halmashauri inatakiwa kuwa na takwimu sahihi za matumizi bora ya ardhi ilikujua maeneo sahihi ya matumizi ya ardhi, kujua namna ya kuhifadhi maji na pia kutoa elimu ya mazingira na uhifadhi wa maji kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Akichangia maoni yake kwa wajumbe wa Kikosi Kazi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbarali Bwana Mathayo Mwangomo amesema kuwa shughuli za kibinadamu hasa kilimo zinachangia kupunguza mtiririko wa Maji kwenda mito hii ni baada ya Serikali kubinafsisha mashamba makubwa ya mpunga mwaka 2006 na wananchi kukosa maeneo ya kulima kilimo cha umwagiliaji.
Bwana Mwangomo amesema kuwa kutokana na uchakavu wa miundombinu na mingine kujengwa kiholela kwa mtindo wa kudaka maji kutoka kwenye mifereji ya matoleo toka kwa wawekezaji na wakulima kunasababisha maji kutorudishwa kwenye mto Mbarali na kupotelea katika mashamba ya wananchi hasa kwenye Vijiji vya Ukwavila, Iyala, Mpunga Mmoja, Imalilo Songwe na Mwendamtitu.
Naye Katibu wa CCM Abdala Mpokwa amesema kuwa Serikali inatakiwa irejee makubaliano yake na wananchi ya kujenga mabwawa ili kuwepo na uvunaji wa maji ya mvua na pia kuiomba Serikali kufanya matengenezo ya miundombinu ya mashamba na hasa mifereji katika Kata za Luhanga, Imalilo Songwe, Ukwavila, Itamboleo na Mwantenga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bwana Kivuma Hamisi Msangi amesema kuwa kuna idadi kubwa ya mifugo katika halmashauri kuliko uwezo wa Wilaya hiyo kuhudumia ambapo maji yanayotumika ni mengi zaidi kuliko rasilimali iliyopo na kuchangia kukauka kwa baadhi ya mito.
Aidha, Bwana Msangi amesema kuwa Halmashauri ina skimu 86 za umwagiliaji lakini ni skimu 5 tu zina matoleo ya maji kurudisha mtoni kwa sababu mifereji mingi ya matoleo haisafishwi mara kwa mara na kufanya magugu maji na uchafu kuzui maji kutiririka kuelekea mitoni.
Aidha, Kikosi kazi hicho kimekuwa na wasiwasi juu ya utekelezaji wa mradi wa Skimu ya Mwendamtitu ambao unahudumia hekta 3000 za kilimo cha mpunga kwa kupoteza maji kwa wingi kutokana na miundombinu ya skimu hiyo kutengen na kufanya wananchi kuchepusha maji kiholela.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa