Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Amour Hamad Amour ameipongeza Halmashauri ya Jiji kwa kuweza mazingira safi ya waalimu na wanafunzi wakati akifungua nyumba moja ya walimu sita (Six in One) na maabara katika shule ya Sekondari Nsoho.
Bwana Amor ameishukuru Halmashauri ya Jiji kwa kufanikisha jitihada za serikali ya awamu ya tano kwa kusogeza huduma za elimu karibu na wananchi na kuwa katika mazingira bora kwa kuweza kujenga nyumba moja ya walimu sita na maabara.
" Maendeleo katika sekta ya elimu yanakuja pale tayari kuna miundombinu mizuri ya kufanya kazi na kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira sahihi na wanafunzi kupata huduma hii kiuraihisi." Aidha, Bwana Amor amesema kuwa uwepo wa maabara unakwenda kuwezesha wanafunzi kusoma kwa vitendo na walimu kuweza kufundisha kwa ari zaidi.
Naye Afisa elimu Sekondari Bibi Lyidia Herbeth amesema kuwa Shule ya Sekondari Nsoho kwa nguvu ya wananchi wa Kata tatu Nsoho Ghana na Iziwa kwa kushirikiana na Halmashauri. Ujenzi ya Jengo la nyumba moja ya walimu sita , Jengo limegharimu jumla ya shilingi milioni mia moja tisini na tatu(193,717,300) Michango ya halmashauri na fedha kutoka serikali kuu kwa kushirikiana na Benki ya Dunia katika utekelezaji wa Mpango Maendeleo ya elimu ya sekondari awamu ya pili. MMES II 184,954,300, Halmashauri imetoa sh. 8,723,000
Bibi Herbeth amesema kuwa Katika utekelezaji wa agizo la serikali la kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na nyumba za waalimu, halmashauri kwa kushirikiana na Serikali Kuu imekamilisha jengo la nyumba hiyo itakayotumiwa na walimu sita kwa lengo la kuboresha mazingira ya walimu wa shule ya sekondari nsoho.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa