Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,
Mhandisi Simeon Shauri amesema utekelezaji mradi mkubwa wa maji kutoka mto Kiwira hadi Mbeya Mjini na na Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi utakaogharimu sh. Bilioni 47 utasaidia upatikanaji wa maji ya uhakika katika maeneo hayo.
Ameleeza hayo katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ya kukagua chanzo cha maji cha mto Kiwira wilayani Rungwe na kukagua jengo la kisasa la mamlaka hiyo.
"Kulikuwa na changamoto kubwa sana ya tatizo la maji katika baadhi ya maeneo Jijini hapa na Mbeya vijijini sasa kupitia mradi huu tuna uhakika wananchi wataondokana na changamoto ya maji."amesema.
Pamoja na mambo mengine Makalla ameagiza watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya kufanya kazi kwa weledi na kujenga mahusiano mazuri na wateja pindi wanapotoa huduma.
"Ninawaagiza uongozi fuatilieni utendaji kazi wa watumishi, wengi wanatoa huduma hafifu lakini kwenye 'kuchart' wako vizuri sana sasa katika hilo ninakemea acheni mara moja na fanyeni kazi ya kuwahudumia wananchi.
Katika hatua nyingine ameiagiza mamlaka hiyo kufanya vipindi katika Vituo vya radio na televisheni ili kuelimisha jamii kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
"Mbeya kuna radio nyingi mnashindwa kuzitumia sasa anzeni mfumo wa kuvitumia kutoa elimu kwa jamii"alisema.
Meneja biashara wa Mamlaka hiyo, Venance Hawela amesema mamlaka hiyo imekuwa ikikusanya mapato ya Sh milioni 800 kwa mwezi na kwamba kuna wateja 52,000 kati ya hao 1,972 ni wa maji taka.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa