Wanafunzi wanaoshiriki Mashindano ya UMITASHUMTA Kutoka Shule za Msingi Mkoani Mkoani Mbeya wameaswa kutanguliza Nidhamu pindi wanaposhiriki Michezo hiyo kwakuwa Siri ya Ushindi wao na Ufauli wao imejificha hapo.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Mr. Emmanuel George ametoa Rai hiyo wakati akifunga Mashindano hayo kwa ngazi ya Mkoa yaliyofanyika Shule ya Sekondari Iyunga Jijini Mbeya na Kutoa Baraka zote kwa Wanafunzi waliochaguliwa kushiriki Michezo ngazi ya Taifa Mkoani Tabora.
"Hakuna Ufaulu Wala Ushindi Unaweza kupatikana bila Kujali Nidhamu hivyo kashindaneni kufa na kupona na Shauku yangu kuona siku mnarejea Mje Mkiwa mmebeba Makombe ya Michezo mtakayoshindania" Amesema George
Kwa Upande wa Maafisa Michezo Halmashauri,Walimu na Wakufunzi(Coaches) amewapongeza kwa jitihada zao za wazi za kuwatengeneza Watoto kimichezo Kisha akawaasa waendelee kujitoa kuwasimamia kwa Ukaribu ili nia ya Mkoa wa Mbeya kuibuka Kinara wa Michezo kama ilivyo kwenye Elimu isipotee.
Robert Mfugale ni Afisa Michezo Mkoa wa Mbeya amemuahidi Mgeni Rasmi kuyasimamia yote aliyoyaagiza na Hana shaka na uimara wa Timu zinazokwenda kuiwakilisha Mbeya katika Mashindano ya Kitaifa "Makombe tutarudi nayo Mh: Mgeni Rasmi Inshallah" alimaliza Mfugale.
Mashindano ya UMITASHUMTA Ngazi ya Mkoa yamemalizika ambapo yalishirikisha Timu Kutoka Halmashauri zote za Mbeya, na Kyela kuibuka Mshindi wa Jumla Licha ya Halmashauri zingine kuibuka Mshindi katika Mchezo Mmoja Mmoja.
Kambi kwaajiri ya Washiriki wawakilishi Kitaifa inaanza Tarhe 29 Mei 2024 hadi Tarehe 4 Mei na Tarehe 5 Timu hiyo itasafiri kuelekea Mkoani Tabora.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa