Mkoa wa Mbeya umejenga jumla ya vyumba vya madarasa 488, nyumba za walimu 16 na matundu ya choo 827 kati ya Mei 2017 na Mei 2018 kwa lengo la kuboresha miundombinu na mazingira ya kutolea elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Akisoma taarifa ya mkoa leo wakati akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Songwe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla amesema kuwa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule unapewa uzito unao stahili.
Mhe Makalla amesema kuwa mkoa umeendelea kusimamia na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuzalisha wataalamu wataklaochangia katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda.
Mhe, Makalla amesema kutokana na utekelezaji wa mpango wa elimu bure na uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya kutolea elimu udahili wa wanafunzi umeongezeka katika ngazi mbalimbali kwa mwaka 2017 na 2018.
Aidha, Kuhusu Vita dhidi ya Rushwa Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa umeendelea kuimarisha mikakati kwa kushirikiana na wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambapo TAKUKURU imeendelea kutoa elimu kwa wananchi 51,747 kwa kipindi cha Julai, 2017 hadi Machi 2018
Jumla ya taarifa 233 za viashiria vya Rushwa zilipokelewa ambapo 146 ziko kwenye hatua ya Uchunguzi, 86 zilifanyiwa kazi na kukamilika, kesi 16 zilifunguliwa Mahakamani zipo katika hatua mbalimbali .
Suala Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe. Makalla amesema Mkoa umeanzisha vituo mbalimbali vya kutoa Elimu kwa Vijana ili watambue madhara ya kutumia Dawa Mbalimbali zakulevya. Kwa mwaka 2017/2018watuhumiwa 341 walikamatwa wakiwa na Heroine gramu 221, amphemine gramu 20, bangi kilo 403 na gramu 480 za mirungi.
Mhe Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa umeendelea kuimarisha utoaji wa huduma za nasaha na upimaji wa hiari kwa vituo vyote Afya vya Mkoa, ambapo hadi kufikia Desemba, 2017 jumla ya watu 496,044 walipima VVU kati yao 26,328 walikutwa na maambukizi ya UKIMWI sawa na asilimia 5,3.
Aidha Mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi kuweka mazingira safi ili kupunguza Mbu wanaoambukiza Malaria. Mkoa umefanikiwa kupunguza maambukizi ya Maralia kutoka wagonjwa 98,835 kwa mwaka 2016 hadi kufikia wagonjwa 98,425 kwa mwaka 2017.
Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mbeya utazindua miradi 28, kuweka mawe ya msingi miradi 13 na kukagua miradi 11 yenye thamani ya thamani ya shilingi 13,693,087,483.75 katika halmashauri zote za mkoa. Kati ya fedha hizo Serikali Kuu imetoa kiasi cha shilingi 9,481,917,770.75, halmashauri shilingi 718,532,228, wananchi wamechangia kiasi cha shilingi 1,649,470,473.00, wahisani shilingi1,837,675,012.00 na fedha za mfuko wa jimbo shilingi 5,492,000
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa