Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema katika kupunguza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa, sasa wataanza kujenga majengo ya ghorofa katika shule za msingi na sekondari za Serikali za mchepuo wa Kiingereza.
Chalamila ameeleza hayo leo Jumatano Desemba 9, 2020 wakati akikagua ujenzi wa ghorofa mbili shule ya msingi Mkapa, kusisitiza kuwa itachangia kupunguza gharama za miradi za ujenzi kila mwaka.
Amesema utaratibu huo utakuwa chachu ya kuondokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule ambazo zina eneo dogo.
Chalamila ameagiza uongozi wa halmashauri ya Jiji kuharakisha mradi huo unakamilika Februari 2021 ili kupokea watoto wengi.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Amede Ng'anidako amesema kwa sasa wanasubiri matokeo ya wanafunzi watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwakani ili kubaini kama kutakuwa na uhaba.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa