Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera amezindua rasmi Zoezi la Ugawaji Vyandarua vyenye Dawa kwa Wanafunzi Mashuleni ikiwa ni sehemu ya Mikakati na Mipango Madhubuti ya kuzuia, kuteketeza na kutokomeza kabisa Maralia kwa Mkoa wa Mbeya.
Vyandarua hivyo vimepokelewa na Maafisa Elimu Kutoka Halmashauri zote kwa niaba ya Wanafunzi na Kisha Zoezi la Uzinduzi na Ugawaji litaendelea katika Kila Wilaya na Halmashauri kwa Usimamizi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwa kishirikiana na Maafisa Elimu.
Zoezi hilo limefanyika Leo katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ambapo RC Homera ameshiriki katika kikao maalumu Cha kujadili, kupokea maoni na kushauri Njia mbadala za kuzuia na kutokomeza Ugonjwa huo hatari unaozidi kuua Maelfu ya Watu Duniani.
Katika Hotuba yake RC Homera amewaasa Maafisa Elimu kutoonyesha Upendeleo wa aina yeyote wakati wa Ugawaji wa Vyandarua hivyo bali Kila Mmoja apate kulingana na taratibu zilivyowekwa na Mamlaka husika.
"Maafisa Elimu Naomba mgawe Vyandarua pasipo Ubaguzi wowote na hizo timu zitakazokuwa zinahusika basi zifanye kazi kwa Njia ya haki ili Kila Mtoto apate chandarua aweze kujikinga na Ugonjwa wa Maralia"
RC Homera amesema Zoezi hili la Ugawaji wa Vyandarua Mashuleni ni Adhima ya Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha inapunguza maambukizi ya Maralia Kutoka Asilimia 8.1 Mwaka 2022 mpaka kufikia kiwango Cha Chini Cha Asilimia 3.5 ifikapo Mwaka 2025.
Kikao hicho kilichofanyika Leo Oktoba 18 2023 kineshirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu Wizara ya TAMISEMI, MSD Taasisi na Viongozi Kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa