Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amezuia safari zote za Watendaji wa Halmashauri Mkoa wa Mbeya mpaka pale watakapomaliza kuanza mpango kazi wa Vipaumbele vya Mkoa.
Mhe. Makalla ametoa katazo hilo hii leo alipokua anafungua kikao cha Baraza Maalumu la kubadili hoja za CAG Halmashauri ya Rungwe.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema kuwa amekataa kutoa kibali cha Watendaji kutoka nje ya Mkoa wa Mbeya baada ya kuona maagizo aliyoyatoa hayatekelezwi na amesema ruhusa zitatolewa baada ya watendaji hao kuwasilisha mipango hiyo.
Akizungumza na Baraza la Madiwani Mhe. Makalla amesema kila Halmashauri unatakiwa kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda kidogo, vya kati na viwanda vikubwa ili yatangazwe kwa ajili ya kuvutia wawekezaji.
"Kila Halmashauri inatakiwa kuchagua mazao ambayo yataitambulisha kwa ajili ya Kujenga viwanda vya mazao hayo ili kuweza kuwawezesha wakulima kunufaika na kazi zao". Mhe. Makalla
Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka piakuwashirikisha Madiwani wakati wa kuandaa maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya viwanda vidogo, kati na vikubwa.
Aidha, amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishali Viazi, Ndizi, Maparachichi, Chai, Maziwa na wajasiriamali kuongeza thamani ya bidhaa zao na kufunga katika vifungaishio vizuri kufanya hivyo kutaongeza soko na mapato ya Halmashauri.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa