Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewataka Wakala Barabara TARURA na TANROADS mkoani Mbeya kusimamia miradi ya baraba ikamilike kwa muda unaopangwa na iendane na thamani ya fedha inayotolewa.
Mhe Makalla ameyasema hayo Mei 5, 2018 alipokuwa akifungua Kikao cha bodi ya barabara mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkapa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Alisema kuwa katika kipindi chote atakachokuwepo Mkoani Mbeya hatakubali Kupokea miradi ya barabara itakayojengwa chini ya kiwango na ambayo haiendani na thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali.
Akiongea katika Kikao hicho Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa (TANROADS) Mhandisi Paul Lyakurwa alisema kuwa Mkoa wa Mbeya umetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 15.118 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa miradi midogo na miradi mikubwa.
Mhandisi jumla ya shilingi Bilioni 57.627 zimeidhinishwa na Serikali mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo shilingi Bilioni 51.827 kwa barabara kuu, shilingi Bilioni 2.076 kwa barabara za Mkoa na shilingi Bilioni 3.724 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Songwe.
Mhandisi Lyakurwa amesema kuwa kumekuwepo na shughuli nyingi za biashara na kilimo kandokando ya barabarab hususani maeneo ya Uyole, Kiwira na Ushirika ambazo zinafanywa kinyume cha Sheria na kuhatarisha usalama wa watumia barabara
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa