9th June, 2020.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Albert Chalamila amefanyamkutano na wananchi wa kijiji cha Isyonje ambacho kipo katikampaka wa Mbeya na Rungwe ambapo wananchi wa kijiji hichowalikua katika mgogoro wa mda mrefu kati yao na TANROADS kuhusu kulipwa fidia ya maeneo yao wanayoishi ambapomwaka 2017 Tanroad iliwapa taarifa wananchi wanaoishi eneohilo la Isyoke kuhama na kuwahidi kuwalipa fidia wananchi waeneo hilo ndani ya miezi 6.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isyoke Mkuu wa mkoaamewaeleza kua Mheshimiwa raisi wa Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania Dr.John P. Magufuli alisikia kilio cha wananchi wakijiji hicho leo asubuhi kupitia radio ya taifa TBC wakilalamikakucheleweshewa kulipwa fidia kwa mda mrefu tangu 2017 walipoambiwa na Tanroad kuhusu eneo lao kutaka kutumikakwa ajili ya ujenzi wa mizani na kuahidiwa kulipwa fidia ndaniya miezi sita lakini mpaka leo hawajalipwa fidia zao hukuwakipewa tangazo la kutoliendeleza eneo lao kwa kujenga nakutakiwa kusubiria fidia. Wananchi hao walitoa kilio chao nakumuomba Mh. Raisi awasikilize kwani nyumba zao zinazidikuharibika na kushindwa kuzifanyia ukaratabati kutokana nakatazo walilopewa na Tanroad. Mkuu wa mkoa alieleza kuaMheshimiwa Rais amemuagiza kwenda kuwapa taarifa Tanroadkuwa eneo hilo la Isyonje libaki kwa wananchi lisichukuliwe,amewataka Tanroad wanapotaka kuchukua eneo lolote la wananchi kwa ajili ya ujenzi wanatakiwa kuwalipa kwanza fidiandani ya miezi sita.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Julius Chalya kushotoakimuonyesha Mkuu wa Mkoa maeneo ambayo Tanroadilipanga kubomoa ili kupisha ujenzi wa mizani katika kijiji cha Isyonje, kulia ni mkuu wa wilaya ya mbeya mjini Mh. Paul Ntinika
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya RPC Ulrich Mateiakizungumza na wananchi wa Isyonje na kuwasihi kuendelezakulinda swala la ulinzi na usalama wa mkoa wa mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa