Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewataka watumishi wa halmashauri ya Kyela kukamilisha kujibu hoja za ukaguzi kabla hajawachukulia hatua za kinidhamu.
Mh. Chalamila ameyasema hayo leo katika kikao cha baraza la madiwani kupitia hoja za ukaguzi na kuwataka kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi watakaokuwa wanatengeneza hoja.
Mhe. Chalamila amesema kuwa ujibuji wa hoja za ukaguzi lazima uwe ni agenda kwenye vikao vyote vya halmashauri na sio kutengeneza hoja mpya.
Amesema kuwa usimamizi wa kanuni na taratibu za matumizi ya fedha na manunuzi lazima vizingatiwe na kusimamiwa ipasavyo na halmashauri
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Katibu Tawala wa Mkoa Bibi Mariam Mtunguja amewataka watumishi hao kutimiza wajibu wao na kuwa na ushirikiano kwenye kujibu hoja kwa idara zote.
Mama Mtunguja amesema kuwa lengo la kikao hivi ni kujua kama fedha za serikali zinazoletwa zinatekelezwa kwa majukumu yaliyo pangiwa na kama thamani ya fedha ipo sawa na huduma inayotolewa.
Mkaguzi Steven Shio kutoka Ofisi ya Mkaguzi Kanda amezitaka kuwa na mfumo sahihi wa kudhibiti mapato kwa wakuu wa idara husika na katika ujibuji wa hoja na kuzipeleka kwenye vikao vya wakuu wa idara ili uwepo umilikicwa hoja
Bw. Shio amesema halmashauri ya Kyela imeonyesha kuwa hakuna ushiriki wa wakuu wa idara katika kutoa majibu ya hoja kuonyesha ni mtu mmoja anayejibu hoja zote.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa