Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 zimezindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 9 ya afya,elimu,Maji, mifugo, barabara na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi iliyogharimu kiasi cha shilingi 3,002,955,550 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu, Wahisani na Wananchi.
Akisoma taarifa ya halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Bi Rowena amesema kuwa miradi 3 imewekewa mawe ya msingi, miradi 4 imezinduliwa na vikundi 11 vya vijana, Walemavu na wanawake vimekabidhiwa hundi na kukaguliwa utekelezaji wa miradi
Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Kyela ni zahanati ya Ilenge, Daraja la Isabula-Landani-Masukulu, vyumba vya madarasa na ofisi sekondari ya Kayuki, vyumba vya madarasa Nuru English Medium, kituo cha kukusanya maziwa na kukagua na kutoa hundi kwa vikundi vya vijana walemavu na wananwake.
Aidha kusuhu kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Rungwe imetekeleza vyema ujumbe huo kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya madarasa, nyumba za walimu, hosteli, majengo ya utwala pamoja na matundu ya vyoo.
Hadi kufikia mwezi Aprili, 2018 kiasi cha shilingi 13,774,500/= kilitumika kukamiliswha madarasa 2, ukarabati wa madarasa 3 na ujenzi wa matundu ya vyoo 24 katika shule za msingi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa