Uongozi wa chuo cha Taifa cha ULINZI ukiwa na maafisa wa jeshi kutoka nchi Mbalimbali wametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Uongozi huo wa chuo cha Ulinzi cha Jeshi umeridhishwa na hali ya usalama na utulivu mkoani Mbeya na jinsi Serikali ya Mkoa inavyosimamia na kuhamasisha shughuli za maendeleo
Wamepongeza Mkoa wa Mbeya kufanya vizuri ktk UCHUMI na kuwa Mkoa wa pili kitaifa na Mkoa wa kwanza ktk mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Aidha, wameridhishwa na uhamasishaji wa viwanda ktk Mkoa wa Mbeya na namna Mkoa ulivyojipanga kuhamisha kilimo na kujitosheleza kwa chakula
Viongozi na Maafisa wa chuo cha ULINZI wapo mkoani Mbeya kwa ziara ya siku 4 watatembelea uwanja wa ndege songwe, baadhi YA viwanda Wilaya ya Mbeya na Mbarali ,Bandari ya Kiwira na Kituo cha Forodha Kasumulu
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa