Mwenge wa Uhuru 2024 kupitia kwa Ndg: Godfrey Eliakim Mnzava na timu yake umekagua na kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Kituo Cha Afya Itunge Kilichoko Kata ya Itunge Halmashauri ya Wilaya ya Kyela na kuwaasa wataalam na Wahudumu ngazi ya Afya kuwa na Kauli Njema hasa wanapowahudumia Wagonjwa.
Mnzava akiwa wilayani Kyela katika Majukumu yake ya kukimbizwa na kumulika Miradi Mbalimbali ya Maendeleo kupitia Mwenge wa Uhuru Amesema Serikali imewekeza Nguvu nyingi kwenye sekta ya Afya hivyo ni Vyema Wahudumu wakawa na Kauli Njema kwa Wagonjwa sambamba na Kuiwekea uangalizi wa Kutosha dhidi ya Watu Wachache wasio na dhamili Njema.
Mradi huo utakaohudumia Wananchi wa Vitongoji vinne Ndani ya Kata ya Itunge na Maeneo Jirani mpaka Sasa umegharimu Jumla ya Shilingi 702,500.000 kwa kujenga Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara, Nyumba ya Watumishi(Three in one), Jengo la Mama na Mtoto, Njia(Walk way) na kichomea taka.
Chanzo Cha Mapato ya Ujenzi wa Kituo hiki ni Serikali kuu ambayo ilitoa 590,000,000 Halmashauri ya Wilaya Sh. 50,000,000 na Nguvu za Wananchi TSH. 12,500,000 na Wadau wa Maendeleo TSH 50,000,000.
Kukamilika kwa Mradi huu wa Kituo Cha Afya utasogeza kwa Karibu huduma za Matibabu ya haraka kwa Kata Tano za Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ambazo ni Itunge, Mwaya, Kajunjumele, Serengeti na Bondeni.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa