Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh: Jaffar Haniu Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Cde: Juma Z. Homera ameongoza Zoezi la Upandaji Miti lililoandaliwa na Ofisi ya Mufti Tanzania kupitia Baraza la Waislam Tanzania(BAKWATA) kama sehemu ya Kuunga jitihada za Serikali za kutunza Mazingira kupitia Kampeni ya Upandaji Miti katika Kila Wilaya.
Mh: Hanniu amezindua zoezi hilo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kutoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya Kulinda na kutunza Mazingira pasipo kushurutishwa na mtu
"Sisi tunapumua kupitia hewa ya Oxygen na Oxygen ni sehemu ya Uhai wetu kwahyo naipongeza saana Ofisi ya Mufti kupitia Baraza la Waislam Tanzania BAKWATA na Uongozi wa Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Mkoa kwa Uratibu Mzuri wa Shughuli hii
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa kwaniaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Msafiri Njalabaha amesema wao kama BAKWATA wameamua kuiunga Serikali katika Kampeni hii ya Upandaji Miti na wamejiwekea Malengo ya Kupanda Miti Milioni Mbili kwa Mwaka hapa Nchini.
"Katika Dini Zetu Tunafundishwa kuwa Mwanadamu akifariki Mambo yake yote yanakoma isipokuwa Sadaka ya Kuendelea aliyoifanya na miongoni mwa Sadaka hizo ni ya Upandaji Miti Ukipanda mti unakuwa umeweka ukumbusho kwa kuyafanyia Mema Wanadamu wenzako Amesema Sheikh Njalabaha."
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi Anna Mwambenee amesema Mti ni Uhai wa Binadamu, Miti ni Matunda, Miti ni Chakula na Miti ikiwepo hali ya hewa inakuwa Nzuri,na Ustawi wa Miti tunapata mpaka Dawa za kuponya baadhi ya Malachi yetu hivyo tunawashukuru kwa Kampeni hii Nzuri nasi tunawaahidi kuitunza Miti hii kamailivyo dhamila ya Serikali Amesema!
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt:Tulia Ackson Amesema Dkt: Tulia ni Moja Kati ya Viongozi wanofurahishwa na Ustawi wa Mbeya katika Kuimarisha Ukijani wake kama ambavyo Mbeya inafahamika kuwa(The Green city) hivyo amezipongeza juhudi za BAKWATA na kuahidi kwaniaba ya Wananchi kuitunza Miti hiyo na kuendelea Kutoa Elimu kuhusu madhara ya Kukata Miti na faida ya kutunza Miti.
Kampeni hii ya Upandaji Miti Kutoka BAKWATA imebeba Kauli mbiu ya Kupanda Miti ni Sadaka yenye kuendelea.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa