Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Ndugu Rodrick Mpogolo amelipongeza shirika lisilo lakiserikali la ESLT FOUNDATION linalojihusisha na upingaji wa utumikishwaji wa watoto ambapo mpogolo amelipongeza kwa jitihada zinazo fanywa na shirika hilo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mbeya, Tabora na Songwe
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau na wakuu wa Taasisi mbalimbali Chenye lengo la kufanya tathimini ya utumikishwaji wa watotokatika mikoa hiyo
Aidha Meneja wa mradi wa Prosper - Reset Fredi Malaso ameeleza namna wanavyoweza kutekeleza mradi huo kwa udhamini wa shirika la ESLT FOUNDATION ambapo amesema lengo la mradi huo ni kupinga utumikishwaji wa watoto katika mashamba ya tumbaku ili watoto waweze kupata haki yao ya msingi ya kutimiza ndoto zao hasa katika Elimu.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho akiwemo Afisa kazi mfawidhi mkoa wa Songwe Eva Lugendo amesema baadhi ya watoto yamekuwa wakitumikishwa katika machimbo ya madini hali ambayo ni kinyume na sheria huku Bonifas Gatyo Afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya kaliua Tabora amewahamasisha wazazi na walezi kuwalinda watoto na kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa