• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Abaini Matumizi Mabaya ya Fedha Ujenzi wa Kituo cha Afya Masukulu

Imetumwa : July 5th, 2019

Na Esther Macha ,Rungwe

UJENZI wa majengo saba ya kituo cha afya cha Masukulu kilichopo wilayani Rungwe umeingia dosari baada ya kubainika  majengo hayo kujengwa chini ya kiwango .

Lakini pia Vifaa vilivyonunuliwa vilikuwa tofauti na  vilivyoidhinishwa kwa ujenzi wwa majengo ya serikali.

Akizungumza Jana Mara baada ya kutembelea ujenzi wa majengo saba ,Mkuu wa Mkoa wa mbeya Albert Chalamila alisema katika ujenzi huo wa majengo hayo kuna wizi mkubwa umefanyika .

Chalamila alisema kituo hicho cha afya cha masukulu ni mfano mchache wa vituo vya afya ambacho kimefanywa kuwa shamba la bibi.

"Nilitaka kufanya maamuzi  hapa lakini mpaka nikasome taarifa ya Takukuru niliyoletewa nitarudi tena hapa kwenye kituo hiki  baada ya siku nne na kwa hali hii lazima tuwawajibishe haiwezekani kabisa Mhandisi halmashauri hajitambui na hata msimamizi wa mradi huu hajitambui"alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Rungwe  ,Mnkondo Bendera   alisema kwamba kilichofanywa na wasimamizi wa ujenzi wa kituo hicho hakuna sababu ya kudanganyana kikubwa wakubali kuwa wamekosa katika mradi huo kwani  kuna wizi wa wazi kabisa hapa Mkurugenzi hukwepi.

Naye Diwani wa kata ya Masukulu ,Weston Mwansasu alisema kilichofanywa kuchelewa kwa mradi huo ni mkurugenzi wa halmashauri kutowajibika katika nafasi yake kwani fedha za ujenzi huo wa majengo toka zimekuja zina miezi mitatu lakini hakuna kazi iliyofanyika mpaka pale taarifa ya ujio wa Mkuu wa mkoa  ilipokuja ndio ujenzi ujenzi ulipoanza.

"Hali ya ujenzi ndio kama unavyoona upo chini ya kiwango kabisa hapa kulikuwa na wizi wa wazi kabisa katika.manunuzi na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri"alisema diwani huyo.

Aidha Mwansansu alisema alipotaka kuhoji kama diwani aliambiwa kuwa ni maagizo kutoka ofisi ya Mkurugenzi kwani magari yaliyokuwa yanabeba mchanga baada ya kushusha wanaambiwa kuwa ni tripu tatu wakati ni moja tu ni wizi wa wazi kabisa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe, Loema Peter alisema walipokea mil .500,kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Masukulu pamoja na Ikuti mil.500 .

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa