Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera leo tarehe 26.04.2022 amefanya ziara katika halmashauri ya Mbeya vijijini na kufungua kituo cha Afya Swaya ambacho kimekua kitua cha kwanza kuanza kutoa huduma ukilinganishana Wilaya nyingine ambacho kwa awamu ya kwanza kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 250 na awamu ya pili ujenzi umeanza kwa majengo ya Mama na mtoto pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti (Mortuary).
Akizungumza na wananchi mbalimbali walio hudhuria ufunguzi huo Rc Homera alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Dc Steven Katemba kwa kazi kubwa anayoifanya katika Halmashairi yake pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali kuhakikisha miradi yote inayoletwa na serikali inakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Dkt Angelina Lutambi alisema kuwa wana Swaya wamepata bahati kubwa ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya na kuwataka kuendelea kumuunga mkono Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ili azidi kuendelea kuwaletea maendeleo zaidi na kuahidi kuendelea kuhakikisha kusimamia Ujenzi na fedha zote alizoleta Mh. Rais zinatumika kukamilisha majengo yote yaliyokusudiwa kwa wakati ili kuweza kuwapatia huduma wananchi.
Mkurugenzi wa Mbeya Dc Steven Katemba kwa upande wake amesema kuna vijiji 140 ambapo katika vijiji hivyo 95 vitakabidhiwa mizani kwa ajili ya kupimia uzito watoto wadogo na kwa awamu ya pili watamalizia vijiji vingine ambavyo vitabaki. Mizani itasaidia kujua upande wa lishe kwa watoto, pia aliweza kugawa vitabu maalum vya mahudhurio ambavyo vitakuwa vikitumika kufanya kazi kila siku kwa ajili ya kutambua idadi ya watoto wenye mahitaji maalum ili kuweza kuwasaidia.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa