Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert amewapongeza wananchi wa kijiji cha Ifupa Wialaya ya Mbeya kwa kuweka utaratibu wa kuwa na harambee kila siku ya Ijumaa kuchangia shughuli za maendeleo.
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua kituo kipya cha afya Ifupa kilichopo kata ya Irungu wilaya ya mbeya vijijini ambavyo kitasaidia kutoa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji hicho pamoja na vijiji vya jirani ambapo kata ya Irungu inavijiji saba.
Chalamila amewapongeza viongozi wa kijiji hicho kwa kuweza kusimamia fedha hizo vizuri na kufanikiwa kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha afya ambacho kitasaidia kutoa huduma mbalimbali katika kijiji hicho
Mukugenzi wa Halmashauri hiyo Ndugu Katemba amesema Halmashauri ya wilaya ilitoa eneo lake ili liweze kutumika katika ujenzi wa kituo hicho kipya cha Afya Ifupa ambapo wananchi wa kijiji hicho pia walichangia michango yao kufanikisha ujenzi huo ambao ulianza tarehe 23/1/2017 lengo ikiwa ni kusaidia wakinamama wajawazito ambao hupata tabu pinda wakitaka kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma za afya karibu.
Katemba ameendelea kuwa wadau mbalimbali wamechangia ujenzi wa kituo hicho cha afya ambapo TANAPA wao walichangia katika ujenzi wa nyumba ya mganga mkuu huku mbunge wa jimbo hilo alitoa mifuko 200 ya saruji
Nae Mbunge wa Mbeya Vijijini Oren Njeza amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa kwa kufungua kituo chao cha Afya ili kiweze kuanza kutoa huduma na kumuomba kwa niaba ya wananchi awafikishie salamu zao kwa Mh.Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa mchango wake mkubwa aliotoa ili kuweza kufanikisha ujenzi huo wa kituo cha afya Ifupa.
Kituo hicho kinawatumishi 6 wa afya ambapo 1 amepelekwa Muhimbili masomoni ili kuongeza ujuzi na kuja kuwapa huduma wananchi mbalimbali katika kituo hicho cha afya.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi wa kijiji hicho kuacha migogoro ili kuendeleza maendeleo ya kijiji hicho huku akiahidi kumaliza migogoro mbalimbali inayo wakabili.
Wananchi wa kijiji cha Ifupa walimshukuru mkuu wa mkoa kwa kufika katika kijiji chao na kuweza kuendesha harambee ambayo kiasi cha fedha walichopata kitaweza kusaidia kukamilisha huduma mbalimbali katika kituo hicho huku mkuu wa mkoa akiwaahidi kurudi tena katika kijiji hicho kuona maendeleo mbalimbali.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa