Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila leo amezindua kituo cha afya katika kijiji cha Ikukwa Wilaya ya mMbeya kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 800 ambazo zimetolewa na serikali kuu ya awamu hii ya tano.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ameridhishwa na utendaji wa Mbunge wa wa Jimbo pamoja Madiwani wake kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa kituo hicho hadi kumalizika,
Mhe Chalamila amesema kuwa ameamua kufika mwenyewe kuona maendeleo katika kijiji cha Ikukwa na kuona Changamoto mbalimbali wanazozikabili wananchi wa kijijihicho ikiwa ni pamoja na tatizo la umeme na kuahidi kuwa kabla yamwezi wa kumi na mbili mwaka huu atahakikisha Umeme umefika katika kituo hicho cha afya, Ameongeza kuwa Mkoa waMbeya umeweza kujenga vituo vipya 19 vya afya katika awamuhii ya tano ya serikali chini ya uwongozi wa Mheshimiwa raisiDr. John Pombe Magufuri ambaye moja ya ahadi zake nikuhakikisha vijiji vyote hapa nchini vinapata umeme.
Mkuu wa mkoa aliendelea kueleza kuwa changamoto nyinginealiyoiyona wakati akiwa njiani ni ubovu wa barabara hadi kufikakatika kijiji hicho cha Ikukwa na kuahidi pia kushughulikiaswala la maji ambalo pia ni changamoto katika kijiji hicho. Aliwaeleza wananchi kuwa vijiji vingi ambavyo vipo katikamipaka hua na changamoto nyingi za mda mrefu ila ataanzakushughulikia swala la Umeme na Maji ili kuzidi kupelekamaendeleo katika kijiji hicho.
Mbeya kuna vijiji 533 na mpaka sasa vijiji 154 tu ambavyo badohavijapata umeme na katika Zahanati hiyo ya Ikukwa serikaliimetenga kiasi cha shilingi milioni 29 laki 6 na tatu elfu 974 ilikukamilisha swala la umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Albert Chalamila akikaguamajengo ya kituo cha afya Ikukwa kabla ya kukizindua rasmi.
Kituo cha Afya Ikukwa
Mbunge wa Mbeya Vijijini Mh. Oran Njezaakizungumza na wananchi.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa