Zaidi Shilingi Milioni 414 za Kitanzania zimechangwa kwenye Harambee iliyoongozwa na Comrade Juma Zuberi Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya Ujenzi wa Ofisi za Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Konde
Harambee hiyo imefanyika leo Oktoba 29 2023 Makao Makuu ya Dayosisi hiyo Wilayani Rungwe Tukuyu ambapo Comrade Homera akiwa Mgeni Rasmi na muongoza Harambee ambapo amelifanya jambo hilo kwa Ukubwa na kuisababishia Matokeo Chanya na Mafanikio Makubwa KKKT Konde.
Kiasi hicho Cha Fedha kimechangwa na Washirika wa Kanisa hilo kwa Kishirikiana na Wadau wa Maendeleo ambapo Ahadi zimepatikana zaidi ya Sh: Milioni 388, Cash zaidi ya Milioni 26 hivyo kukamilisha hesabu ya Zaidi ya Milioni 414 Njee ya Mifuko 150 ya Saruji, Trip 2 za Kokoto na Trip 5 za Mchanga ambazo pia zimechangwa.
Askofu wa Dayosisi ya Konde Geoffrey Mwakihaba amemshukuru RC Homera kwa Kazi kubwa aliyoifanya huku Shukrani za kipekee akizielekeza kwa Dkt: Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kudumisha Amani ya Nchi hasa katika maswala ya Kidini na Kiimani.
Mwakihaba amesema Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde litaendelea Kumuombea Dkt: Samia Suluhu Hassan na Kutoa ushirikiano wa Dhati kwa Serikali nzima ya Tanzania.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa