Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa kipindi cha miaka miwili ukimhusisha bwana Mahenge na Bi Rehema.
Mgogoro huo ulioleta taswira mpya mara baada ya kutolewa taarifa na vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusiana na malalamiko ya bibi huyo ambeya aliweza kupita katika ofisi mbalimbali za serikali ili kuomba msaada.
Homera amesema chanzo cha mgogoro huo ni Bi Rehema alikuwa analima katika shamba la mzee Mahenge kwa kipindi cha muda mrefu baada ya kuazimwa na Mzee Mahenge ili afanye shughuli zake za kilimo cha mahindi na mazao mengine mbalimbali ambapo baada ya kulitumia shamba hilo kwa muda mrefu ndipo ilipofika kipindi mzee Mahenge alihitaji shamba lake ili aweze kulitumia.
Aidha kwa kipindi hicho Bi Rehema alikuwa tayari ameshapanda mazao yake na akiwa anasubiria ili aweze kuvuna ambapo Mzee Mahenge aliona itachukua muda mrefu na kufyeka mazao hayo ili aweze kulitumia shamba lake na kupelekea uharibifu mkubwa shambani hapo ndipo Bi Rehema alipoamua kuchukua hatua ya kwenda kushitaki sehemu mbalimbali za Serikali ili kuweza kupatiwa msaada.
Pia aliweza kufika Dodoma wakati Mh Rais akihutubia katika mkutano mkubwa wa wazi ambapo aliweza kupata nafasi ya kutoa malalamiko yake na kuomba msaada asaidiwe. Mh Raisi alitoa agizo Bibi huyo asaidiwe ili aweze kupata haki yake ambapo tathmini iliweza kufanyika na Mkoa wa Mbeya na ilionyesha ni Kweli mzee Mahenge alifyeka mazao ya Bibi huyo na kupelekea hasara kubwa.
Homera amemkabidhi Bibi huyo kiasi cha shilingi milioni 13 mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na Kamanda na Polisi Mkoa wa Mbeya ambapo Bibi huyo aliweza kwenda kuhifadhi katika Benki.
Amewataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi katika jambo lolote na kuwasihi kufata sheria za nchi ili kujiepusha na matatizo mbalimbali yanayoweza kuwakabili.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa