Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera amewashukuru Wanawake nchini kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo. Hayo ameyazungumza leo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake yaliyofanyika kimkoa katika Mji Mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya.
Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mbeya Homera amesema Tanzania ni miongoni mwa wanachama wa Umoja wa Mataifa na inaungana na Mataifa yote Duniani katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
"Tunaadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwa lengo la kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapokwenda kwa fikra pevu za Kiutamaduni na kisiasa, kijamii na kiuchumi kwani Mapambano dhidi ya ukatili wa Wanawake na Watoto yanaendelea" alisema Homera
Homera ametoa agizo kwa Magereza yaliyopo Mkoani Mbeya ambayo yanatoa mafunzo ya Ufundi, Ujasiliamali kwa wafungwa, ambapo wafungwa wote ambao watakuwa wanatoka Gerezani hasa Wanawake wapewe mikopo ya asilimia 10 ili iweze kuwanufaisha katika maisha yao kwa kuwa watakuwa wameshakuwa watu wema. "Ni muda wa kuwawezesha Mikopo itasaidia kuinua maisha yao" alimaliza Mhe. Homera
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa