Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera ametoa wito kwa Jeshi la Magereza Mkoani Mbeya Kwa Wafungwa ambao wanakidhi Vigezo vya Kuachiwa kuwaharakishia Rufaa zao ikiwezekana kuachiwa kwa Mjibu wa Sheria na Utaratibu wa Parole kama ambavyo imeelekezwa.
Homera ameyasema hayo Leo wakati akizindua Bofi ya Parole Mkoa wa Mbeya kupitia Jeshi la Magereza ambapo amewataka Wajumbe wa Bodi hiyo mkuwa Makini wakati wa kutekeleza Majukumu Yao na kutumia zaidi Busara na hekima kwakuwa watakuwa wanagusa Haki za Wafungwa Moja kwa Moja.
RC Homera ameongeza kuwa ni Vema Wajumbe wakamtanguliza MUNGU mbele wakati wote na kuweka Maslahi mbele na nia Njema ya Taifa kwani kufanya Kwao hivyo watakuwa wanamsaidia Mh: Rais Dkt: Samia Suluhu Hassan Kutekeleza maono yake katika Utendaji wa Haki.
Awali RC Homera amempongeza Waziri na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuridhia Ombi la Uundwaji wa Bodi ya Parole ambayo ndiyo yenye Mamlaka ya kisheria ya kupokea mapendekezo Kutoka kwa sekretariati ya Parole Mkoa na kuyapitia na baada ya kujiridhisha kuwaruhusu Wafungwa hao kunufaika.
Akisoma Risala mbele ya Mkuu wa Mkoa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Lazaro William Nyanga Amesema Bodi hiyo itadumu kwa Miaka mitatu na itatenda Kazi Chini ya Bodi kwa Kushirikiana na Uongozi wa Magereza Mkoa wa Mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa