Homera amesema kuwa mkoa hauko tayari kupiga marufuku mabasi madogo maarufu kama ''hakuna kulala'' kusafirisha abiria kwenda mikoani na kwamba hatua hiyo itachangia kushuka kwa mapato ya mkoa.
''Siwezi kupiga marufuku Mabasi ya hakuna kulala kwani yanachochea uchumi kutokana na shughuli za kiuchumi kwa wafanyabishara sasa tunachofanya ni kuzungumza na wamiliki ili kuingia mkataba na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi,'' amesema.
Amesema kuwa Serikali imekuwa ikitegemea mapato kutokana na shughuli za kiuchumi hivyo kama mkoa utalazimika kuona vibali vinatolewa kwa wawekezaji wa mabasi makubwa na kuhakikisha abiria wanakuwa salama.
''Tunataka mfanyabishara anaondoka jioni jijini Mbeya leo jioni na alfajili yupo Dar es- Salaam anafunga mzigo ananza safari ya kurejea Mbeya na kuendelea na shughuli za uzalishaji,'' amesema Homera.
Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra), Denis Saudi amesema wamepokea maagizo hayo na kwamba wanasubiri maelekezo kutoka Latra makao makuu ili kuanza utekelezaji wa utoaji wa vibali vya kusafirisha abiria nyakati za usiku.
Amefafanua kuwa hivi karibuni kulikuwepo na utaratibu wa utoaji wa vibali kwa mabasi yanayofanya safari za mchana kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam lakini vimesitishwa kutokana na sababu za kiusalama.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa