Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbarali kumkamata mara moja mganga wa tiba za asilimaarufu kama (rambaramba) kwa madai kuendesha shughuli zake kinyume cha sheria kwa lengo la kuondoa wadudu wanaodaiwa kumwagwa kwa njia za kishirikina katika Kata ya Igurusi.
Mhe Makalla, alitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara , baada ya kuusikiiza malalamiko ya wananchi waliyodai kushamili kwa vitendo vya kishirikiana hususan wanaume kungiliwa kinyume cha maumbile na kumwagwa kwa wadudu hao jambo lililowalazimu kuchanga fedha na kumleta mganga huyo.
Mhe Makalla alimwagiza Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama kuweka kambi katika kata hiyo sambasamba na kumtia nguvuni mganga huyo na wananchi walioshiriki kuhamasisha michango.
Wakiongea katika Mkutano huo wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa wamechoshwa na ushirikina uliopo na kwamba umefikia wakati hata wanandoa wanaingia katika na migogoro inayotokana kuingiliwa kimwili kwa njia za kishirikina.
"Tatizo ni kubwa pia kuna wanafunzi wamekuwa wakizimia na kupoteza fahamu,mauaji ya kinyama,watoto kupotea katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa mifupa maporini" alisema Jerat Mwambusi.
Lucas Mwakasege aliomba serikali, viongozi wa dini,mila na machifu kushirikiana kukemea vitendo hivyo kwani vinachangia kushuka shughuli za kiuchumi na jamii kugoma kuchangia miradi ya maendeleo.
"Msema kweli mpenzi wa mungu hawa wadudu, sasa ni mwezi hata tukipulizia dawa hawafi yani hatulali usingizi pia unakuta wanandoa asubuhi mkiamka mnakuta mmeingiliwa vibaya sana "alisema.
Mchungaji wa kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT) ushirika wa Mbarali Yoma Moses alisema kuwa wanakemea vitendo hivyo na kuomba wananchi wamche Mwenyezi Mungu ili visijirudia na kuondokana na imani potofu za kishirikina
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Reuben Mfune alisema kuwa utekelezaji wa agizo hilo unaanza mara moja na kuwataka wananchi kutoitupia lawama Serikali kutokana na vitendo vya mauaji.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa