• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Serikali ya Malawi Yakabidhiwa Msaada wa kutoka kwa Rais

Imetumwa : March 21st, 2019

Na Grace Mwakalinga, Karonga Malawi

MSAADA wa Tani 200 za Mahindi na Tani 15 za Dawa, Magodoro na Vyandarua ambao umetolewa na Rais Dk. John Magufuli kwa watu walioathirika na mafuriko nchini Malawi umewasili na kukabidhiwa kwa Serikali ya Malawi kwa ajili ya kuwafikishia waathirika wa maafa hayo.

Malori manane ambayo yalibeba Shehena ya Tani 200 za Mahindi na moja lililosheheni dawa, Magodoro na Vyandarua yaliwasili wilayani Karonga yakitokea  Tanzania yakitumwa na Rais Dk. John Magufuli .

Msaada huo ulikabidhiwa juzi  nchini Malawi  na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya , Wiliam Ntinika ambaye aliiwakilisha Serikali ya Tanzania.

‘’Tunakabidhi msaada huu ambao umetolewa na Rais  Magufuli nchini  kwa  Rais wa Malawi Mutharika tani 200 za mahindi, dawa, magodoro na vyandarua msaada huu  tunaihakikishia serikali ya Tanzania msaada umeufika hapa Malawi ukiwa salama’’, alisema Ntinika.

Hata hivyo msafara  huo wa  malori kuelekea Wilaya ya Karonga, nchini Malawi uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta ambaye alisema kuwa msaada huo ni alama ya upendo na undugu uliopo baina ya Tanzania na Malawi

Alisema Serikali ya Tanzania ilitoa msaada huo kutokana na  kuwepo kwa mahusiano mazuri baina ya wananchi wa Malawi na Tanzania na kusisitiza kuendelea kushirikiana kwa nyakati zote.

Akipokea  Msaada huo kwa Niaba ya Serikali ya Malawi, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalonga, Raphael Mkisi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa msaada huo huku akisema kuwa Wilaya 13 kutoka mikoa Saba ya Malawi zimeathirika na mafuriko hayo  ambayo yamesababisha zaidi ya watu 60 kupoteza maisha.

Mkisi alisema msaada huo mkubwa utasaidia kuzipa pengo la uhitaji ambalo limetokea kwa sababu ya mafurikio hayo ambayo mbali na kusababisha vifo pia yameharibu miundombinu ya barabara na majengo nchini humo.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa