Wananchi wa Kijiji Cha Iheha kata ya Madibila Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, wameondokana na shida ya maji iliyo watesa Kwa muda mrefu Kwa kutumia maji ya mto pamoja na Mifugo, baada ya mradi wa millioni 800 kukamilika na kuanza kutoa huduma Kwa wakazi wa Kijiji hicho na Kata ya Madibila Kwa ujumla.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera Wananchi wa Kata hiyo Wamesema Mwanzo walikuwa wanachimba Maji chini kwenye mchanga maeneo ya Mtoni waliokua wanatumia na Mifugo Kwa pamoja lakini baada ya Ujio wa Mradi huo umekua mkombozi kwao kupata huduma ya maji Safi na salama.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Homera amewataka Wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kuwa wabunifu pindi serikali inapo sogeza miradi maeneo ya vijijini Kwa kutumia fedha vyema na kusambaza huduma ya maji Kwa eneo kubwa Kama ilivyo adhma ya serikali ya kumtua mama ndio kichwani Kwa kumsogezea huduma ya maji karibu.
Aidha Homera amewataka RUWASA kuomba matumizi ya fedha zaidi ya Milioni 40 zilizobaki katika Ujenzi wa Mradi wa Maji Kijiji Cha Iheha Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali zitumike kusambazwa Maji katika Vitongoji Vingine ili kumaliza kabisa Tatizo la Maji katika kata hiyo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa