Agizo la Raisi latekelezwa na Tanroad, wakabidhi milion 20 kwa mkuu wa Mkoa Kukamilisha ujenzi wa madarasa Isyonje.
10th June,2020
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila leo amepokea kiasi cha shilingi milion 20 kutoka kwa meneja wa Tanroad mkoa wa Mbeya ikiwa ni maagizo yaliyotolewa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John P. Magufuli aliyewataka Tanroad kuchangia kiasi hicho katika kijiji cha Isyonje kutokana na kutoridhishwa na Tanroad mkoa wa Mbeya kwa kuwacheleweshea kuwalipa fidia wananchi wa kijiji hicho ambao walitakiwa kupisha ujenzi wa mizani katika makazi yaowanayoishi.
Jana katika kikao cha Mkuu wa mkoa na wananchi wa Isyonje aliweza kuzungumza moja kwa moja kwa njia ya simu na Mh Raisi ambapo Mh.Raisi alitoa maagizo kwa meneja wa Tanroad wa mkoa wa mbeya kuwapatia milion 20 serikali ya kijiji hicho ili kukamilisha ujenzi wa madarasa pia Mh. Raisi alitengua uwamuzi wa Tanroad kuwahamisha wananchi wa Isyonje ambao walitakiwa kuhama ili kupisha ujenzi wa mizani tangu mwaka 2017 bila kupewa fidia yao na kuamuru wananchi hao waachwe katika maeneo yao na Tanroad watafute eneo jingine.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isyonje leo wakati wa makabidhiano wa fedha hizo Mkuu wa mkoa amemtaka mkuu wa wilaya Rungwe Mh. Julius Chalya kusimamia fedha hizo kwa umakini ili ziweze kutumika kukamilisha ujenzi wa madarasa kama zilivyo kusudiwa na Raisi. Nae mkuu wa wila ya Rugwe alimshukuru Mh.Raisi kwa kuwapatia kiasi hicho ambapo amemuahidi mkuu wa mkoa kuzisimamia fedha hizo kikamilifu ili kukamilisha ujenzi wa madarasa. nae mtendaji wa kijiji cha Isyonje baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Mkuu wa wilaya amesema fedha hizo zitawekwa katka account ya shuleili zitumike katika kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Albert Chalamila akimkabizikiasi cha shilingi milioni 20 mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Julius Chalya kilichotolewa na Tanroad.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Julius Chalya akizungumza 1wananchi wa kijiji cha Isyoke
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya RPC Ulrich Matei akizungumza na wananchi wa Isyonje akiwasisitiza kuendelea kutoa ushirikiano na vyombo cha ulinzi na usalama ili kuweza kutoa taarifa za uhalifu.
Wananchi wa kijiji cha Isyonje wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Mbeya alipo fanya ziara katika kijiji hicho na kukabidhi milioni 20 ili kukamilisha ujenzi wa madarasa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa