Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali katika kusimamia ubora wa bidhaa na kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa feki.
Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo alipokuwa anafungua mafunzo ya wajasiriamali kutoka mikoa Mbeya, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango.
Chalamila amesema kuwa Shirika la TBS si kitu kama litaweza kufanya kazi pekee yale lazima lifanye kazi kwa mashirikiano na taasisi kama TFDA, SIDO au Jeshi la Polisi kwa sababu kuna watu wanaopenda kutii sheria kwa shuruti.
Aidha, amewaambia wajasiriamali wanaopata mafunzo wana kazi nzito ya kuendeleza viwanda vyao na kazi kubwa ya kutoka kuitwa wajasiriamali wadogo kwenda wajasiriamali wakubwa.
Amewataka wajasiriamali hao kufanya biashara zao kwa kufuata taratibu na sheria na kuepuka kuendelea kutoa rushwa kwa baadhi ya watendaji wasio waaminifu kwa sababu watakuwa katika mazingira magumu ya biashara zao.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dk. Yussuf Ngeya amesema mafunzo haya yanafanyika kikanda Mkoa wa Mbeya kwa lengo la kutoa elimu kwa wajasiriamali namna ya kuongeza Viwango vya bidhaa wanazozalisha.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa