Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imeridhishwa na Majibu/Maelezo kuhusu Mapendekezo ya ugawaji Jimbo la Mbeya Mjini Kutoka kwa Wadau wa Uchaguzi wilayani Mbeya na kuahidi kuyapeleka Maelezo na Mawazo yao kwa uongozi wa juu kwaajiri ya Utekelezaji zaidi.
Katika Kikao Maalumu kilichoongozwa na Mwenyekiti Mhe.Magdalena Rwebangira Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, Wadau wa Uchahaguzi wamekiri mbele yake kuwa mapendekezo yaliyopelekwa Tume juu ya ugawaji wa Jimbo hilo yako sawa.
Mapendekezo ya ugawaji wa Jimbo yaliyopelekwa yanaeleza Namna Wadau na Wananchi wanachotaka Jimbo la Mbeya Mjini kuzalisha majimbo Mawili(Jimbo la Mbeya Mjini litakalokuwa na Jumla ya Kata 23 na Jimbo la Uyole litakalokuwa na Jumla ya Kata 13).
Kwa Mjibu wa Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Bi Giveness S. Aswile Amesema mapendekezo ya Jumla ya Kata na mgawanyo wake ni kuwa Jimbo la Uyole lina Kata za,Mwansekwa, Ilemi, Isyesye, Itezi, Ilomba, Iganjo, Iduda, Igawilo,Tembela, Mwasanga,Mwakibete, Nsalaga na Uyole,
Na Jimbo la Mbeya Mjini litakuwa na Kata za Iziwa, Itende, Iwambi, Iyunga, Iyela, Isanga, Itiji, Iganzo, Itagano, Nsoho, Ghana, Sisimba, Maendeleo, Nonde, Majengo, Mbalizi Road, Sinde, Maanga, Ruanda, Mabatini, Forest, Nzovwe, Kalobe.
Aidha Kikao hicho pia kimehudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Z. Homera, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Beno Malisa na Viongozi mbali mbali wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mh. Dormohammed Issa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa