Mkuu wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ameutaka Uongozi wa Chuo cha VETA Kanda kuangalia namna watakavyoweza kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi sehemu nyingine kwa sababu mahitaji yake ni makubwa sana hasa katika kuelekea uchumi
Mhe. Chalamila ameongea hayo leo kwenye ziara ya kukagua na kuongea na watumishi wa chuo hicho na kuwataka kuendelea kuwa na mpango wa kuhakikisha kila fundi aliyeko mtaani amepitia mafunzo katika chuo hicho.
" Nina mpango kabla ya mwaka 2020 kuanzisha mfumo utakaohakikisha fundi yeyote aliyepo katika Mkoa wa Mbeya ana Cheti cha VETA kwa kozi za muda mfupi na Chuo pia muangalie jinsi ya kupunguza ada ili iwe rafiki kwa vijana wote kuweza kulipa". Mhe. Chalamila
Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amekitaka Chuo cha VETA kuwa na mahusiano mazuri na vyuo binafsi vya ufundi na lazima wawe wadhibiti ubora wa taaluma wa vyuo hivyo
Akisoma taarifa ya Chuo hicho Mkuu wa Chuo Cha VETA Mbeya Mhandisi Hasan Kalima amesema kuwa chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali za muda mfupi na muda mrefu ambazo zimeweza kutoa fursa kwa watu wengi kupata mafunzo ya ufundi stadi na kuweza kujiajiri
Mhandisi Kalima amesema wahitimu wa mafunzo ya kozi za muda mfupi kwa muda wa miaka mitano iliyopita imefikia 7,500 katika yao Wanaume 6,000 na Wanawake 1,500 kutokana uhitaji mkubwa uliopo sasa hasa katika elimu ya ujasiriamali
" Chuo kimeweza kujenga Green House kama shamba darasa ili jamii inayotuzunguka iweze kujifunza namna ya kujenga na kutumia kilimo hiki kwa kustawisha mazao mbalimbali". Mhandisi Kalima
Aidha Kalima amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuweza kukitembelea chuo hicho kujionea shughuli za mafunzo na huduma wanazozifanya na kutoa ushauri wa kuboresha
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa