Wafugaji halmashauri ya Wilaya ya Mbarali watakiwa kuvuna mazao ya mifugo na kujishughulisha na shughuli zingine za kiuchumi kama kuanzisha viwanda vya mazao ya mifugo ili kuondokana na ukosefu wa maeneo ya malisho
Hayo yametolewa na timu za wataalamu wa elimu ya uhifadhi na ujirani mwema kwa wananchi wa Mbarali
Afisa Mifugo wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Samora Mshang'a amebaini kuwa Wafugaji wanakuwa na changamoto mbalimbali kama uhaba wa maeneo ya kufugia,ukosefu wa elimu ya ufugaji sheria na miongozo mbalimbali, kutokujua haki za mifugo yao na ukosefu wa masoko ya mazao yao.
"unatakiwa kufuga kwa kujipatia faida na kufuga kwa tija ili kupata maarifa mapya Watumie mifugo yao kwa kujiendeleza kiuchumi na kufuga kwa faida" Mshang'a
Bw Mshang'a amebaini njia Mbalimbali zinazoweza kuwasaidia wafugaji pamoja na kuandaa maeneo ya ufugaji na maeneo ya malisho, kupata maeneo ya maji, kudhibiti magonjwa yanayoweza kudhuru mifugo
Daniel Kamwela Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Mbaralia amewataka wafugaji kutenga maeneo ya kulishia mifugo na kuboresha maeneo ya malisho ambayo tayari halmashauri ya wilaya iliyatenga kwa ajili malisho
Aidha Bw Kamwela amewashauri wafugaji kuanza kuvuna mifugo ili iwanufaishe na kuwekeza mahali mengine na kuanza kufuga mifugo iliyo bora .
"Ni wakati wa kuanza kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji na kuanza kuzuia uingizaji wa mifugo mipya katika vijiji vyao " Kamwela
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa