• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waitara Azindua Maonesho ya NaneNane Mbeya

Imetumwa : August 3rd, 2019

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mwita Waitara  amewataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kuhakikisha ubora wa mazao  na ufugaji unaonekana kwenye mabanda ya  maonyesho  nanenane unafika mpaka kwenye ngazi ya vijiji nchini.

Waitara alitoa agizo hilo alipohutubia washiriki wa maonyesho  ya wakulima maarufu kwa jina la Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwenye Uwanja wa John Mwakangale wakati alipozindua rasmi leo (Jumatano).

Awali kiongozi huyo alikata utepe kwenye geti kuu la kuingia viwanja hivyo na pia alitembelea mabanda mbalimbali ambapo alijionea bidhaa zinazoonyeshwa ikiwamo mifugo hai.

“Nimetembelea mabanda mengi yakiwa na mifugo naa mazao bora  huku mengine yamesindikwa  jambo ambalo sasa naagiza sura ya mabanda  haya ifike hadi vijijini.  Huko vijiji kuwe na mbegu bora, mbolea na mazao yalimwe kwa kufuata kanuni bora za kilimo kama inavyoonekana kwenye mabanda hapa’’ alisema.

Alisema vijana wasaidiwe ili walime kisasa na wapate tani saba hadi 10  za mahindi kwenye ekari moja badala ya tani 2 huku wafugaji wa ngombe wakipata lita 22 kwa siku badala ya lita sita za maziwa.

Waitara aliwataka viongozi wote wa mikoa, wilaya, ,halmashauri  na vyuo vya kilimo kuwasaidia vijana na wanawake katika kuboresha kilimo, ufugaji na uvuvi ili kufika malengo ya Serikali kuhusu uchumi wa viwanda.

“Hakikisheni pembejeo zinapatikana kwa wakati na kwa gharama nafuu  hususan mbegu bora na mbolea ‘’ alisema huku akiwataka pia wakurugenzi wa halmashauri kuwasimamia vizuri maofisa ushirika ili wasiwe chanzo cha migogoro kwenye vyama vya ushirika.

Kuhusu suala la uchaguzi  wa Viongozi wa Serikali za Mitaa , Waitara aliwataka wakazi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kuwachagua viongozi wenye nia ya kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo.

Alisema Rais John Magufuli ameonyesha njia kwa Watanzania kujiletea maendeleo  jambo ambalo watu wanaotaka uongozi wa Serikali za Mitaa lazima walitambuena kuwa tayari kutekeleza.

Awali , Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akizungumza kwenye hafla hiyo alisema viongozi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe, Mbeya, Katavi na Rukwa wamejipanga vema kuongeza kasi ya kusimamia kazi za kilimo, ufugaji  na uvuvi kutekeleza vema masuala ya uchumi wa viwanda.

Chalamila alisema maonyesho hayo yanazidi kuwaunganisha  viongozi wote na wananchi katika kutekeleza vema mkakati wa kutokomeza umasikini nchini.

Maonyesho hayo yanazidi kushika kasi  na yanatarajiwa kufungwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Mizengo Pinda.


Imeandaliwa na Kitengo cha Habari kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya nanenane kanda ya Nyanda za Juu Kusini 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC DKT. HOMERA AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI NNE AFRIKA

    May 26, 2025
  • "WAFUNDISHENI PIA ULAJI WA LISHE WATU MAOFISINI" - RC DKT. HOMERA

    May 26, 2025
  • FISTULA INATIBIKA, MATIBABU NI BURE, KARIBU UHUDUMIWE - DKT. HOMERA

    May 19, 2025
  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa