MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ametoa muda wa juma moja kwa Halmashauri za wilaya mkoani hapa kuandaa mikutano ya wenyeviti wa vijiji ili kuwapa mchanganuo wa utekelezaji wa mradi wa Umeme kupitia wakala wa Umeme vijijini(REA).
Makalla ametoa agizo hilo wakati wa kusikiliza lkero za wananchi Halmashauri ya katika ukumbi wa wa Halmashauri hiyo
Makalla amelazimika kuyasema hayo kufuatia malalamiko mengi yaliyowasilishwa na wananchi kwenye mikutano mengi yakionesha wananchi kuwa na uelewa mdogo juu ya utekelezaji wa mradi wa REA.
Kutokana na uelewa huo mdogo baadhi ya wananchi wamekuwa wakitapeliwa na watu wanaoiitwa vishoka huku wengine pia wakibaki wakilaumu kuofikiwa na mradi au vijiji vyao kurukwa wakati havikuwa katika awamu zilizopita za REA.
Makalla amesema wenyeviti wa vijiji wanapasawa kupewa uelewa wa mradi husika ili na wao waende kuwaelimisha wananchi wao ili kusiwepo na sintofahamu tena juu ya mradi husika.
Amesema licha ya mradi kuingiliwa na matapeli pia kumekuwepo na malalamiko ya Mradi kutozifikia taasisi za kiserikali hususani Shule na Zahanati jambo linaloonekana ni ukiukwaji wa maelekezo ya Serikali kwenye mradi huo.
Awali akiwasilisha kero mmoja wa wakazi wa kijiji cha Syukula kata ya Kyimo wilayani hapa, Timoth Kaswaga amesema wananchi wa kijiji hicho wanahitaji umeme wenye nguvu ya kutosha kwakuwa wanatarajia kujiunga katika vikundi ili waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kuongeza thamani kwenye mazao kabla ya kuyauza.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa