Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amewataka watafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole kutokatishwa tamaa na maneno ya baadhi ya watu ambao hawana taaluma ya tafiti kwa sababu hatuwezi kufanya jambo lolote bila ya kuwa na matokeo ya utafiti.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Kilimo, Mifugo pamoja na Chuo cha Kilimo na kuwataka kuendea kufanya Utafiti zaidi kujikita kutoa tafiti zitakazowasaidia watu wa hali ya chini.
" Watafiti msife moyo hata kidogo kabisa kwa sababu sisi wanasiasa hatukunyang'anyi haki ya kuwa mtafiti ila kuna uwezekano sisi hatutumii matokeo ya utafiti na kwa sababu hiyo watu wanatoa hitimisho la kuwakatisha tamaa". RC Chalamila
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema lugha inayowekwa kwenye tafiti nayo ni tatizo ambapo tunafanya tafiti kwa kumuangalia mtu wa chini wa Tanzania lakini kwa mawazo ya mataifa mengine kwamba watu wa nje wakielewa vizuri basi ndio utafiti mzuri.
Naye Mkurugenzi wa TARI Uyole Dkt Tulole Bucheyeki amesema kuwa taasisi imefanikiwa kuweza kupima udongo na kutoa ushauri kwa wakulima mazao yanayoweza kulimwa katika udongo unaopimwa
Dkt Bucheyeki amesema kuwa majukumu ya taasisi yao ni Kufanya tafiti mbalimbali za Kilimo, kusimamia ubora wa tafiti za kilimo, kushirikiana wataalamu mbalimbali wa ndani na nje kuhuhisha teknolojia na kutafuta fedha za utafiti na kubuni na kuzalisha mbegu za madaraja yote.
Aidha, kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifugo Dkt Suleiman Nasib Masola amesema taasisi hiyo inajukumu la kufanya utafiti wa malisho ya mazuri zaidi ya mifugo , tafiti za magonjwa ya Mifugo ambayo pia yatamuambukiza binadamu na Mifugo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa