Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh:Jaffar Haniu amewaagiza Watendaji wa Mitaa na Wenyeviti kuhakikisha wanasimamia kwa Ukaribu Ustawi wa Miti iliyopandwa Leo na kutosita kumchukulia hatua Kali za Kisheria yeyote atakayehusika kuharibu Mazingira kwa Kukata au kung'oa Mti katika Maeneo Yao.
Haniu ameyasema hayo Leo siku ya Kumbukizi ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika wakati akiongoza Zoezi la Upandaji Miti Mlima Kawetire, Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya akisimama kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa Cde:Juma Z.Homera.
Katika Zoezi hilo lililojumuisha Taasisi mbali mbali, Vyombo vya Usalama na Wananchi wa Kata hiyo DC Haniu amewataka pia Watendaji na Wenyeviti hao Kushirikiana kwa Karibu na Wananchi, kadharika TFS na Uongozi wa Mkoa kuhakikisha Mazingira yanalindwa Vyema.
Kwa Upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa Bi Anna Mwambene amesema zaidi ya Miche Elfu Tatu(3000) leo imepandwa Mlima Kawetire ulioko Kata ya Itezi licha ya Malengo Kimkoa ya Upandaji miti kwa Kata ya Itezi ni Miche Elfu Tano(5000) na kubakiwa na Deni la Miche Elfu Mbili pekee.
Diwani wa Kata ya Itezi Wakala: Shitambala amewaomba Wananchi wa Itezi Kupanda Miti zaidi saana Miti ya Matunda ili mbali na utunzaji Mazingira lakini pia watajipatia Chakula Cha Matunda na kujiongezea Kipato.
Kadharika ameiomba Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa vile viwanja ambavyo Wananchi walipewa lakini bado viko wazi havinajrngwa wavichukue wawape wanaohitaji Kujenga la sivyo Maeneo hayo Uongozi wa Kata upewe wapande Miche ya Maparachichi.
Balozi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya Chief Rocket Mwashinga amesema
Mfano sisi Mazingira yetu ni Mazuri saana hakuna Mtu anayekata Miti kwenye Misitu yetu ya kutambikia hakuna binadamu anayeingia zaidi ya Panya tuu. Sasa tunaomba mwasisitize Wenyeviti wa Mitaa waache mara Moja Tabia ya Kutoa vibali vya Kukata Viti Laa sivyo tupeni ruhusa sisi Machief tulisimamie hili kama Nyie mmeshindwa" amesema Mwashinga ambaye ni Chief wa Kabila la Kisafwa Mbeya.
Mkoa wa Mbeya umeweka Malengo ya Kupanda Miti Milioni Kumi na Laki Tano(10,500,000)kwa mgawanyo wa Kila Halmashauri Milioni Moja na Laki Tano.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa