Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Suleiman Jaffo, amefurahishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwenye Hospitali Mpya ya Wilaya ya Mbarali iliyogharimu kiasi cha tsh. billion 1.5 ambazo zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Jaffo amezitoa pongezi hizo siku ya tarehe 14/12/2019 alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo iliyopo kata ya Lugelele kitongoji cha Mpunga.
*Leo hii nimekuja kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa ujenzi wa hospitali hii, nikiwa kama waziri wenu ambae nimepewa dhamana ya kusimamia wizara hii, hapa nimelidhika sana, hapa hamjanitia hasira, muda sio mrefu nitawaletea milioni 500 nyingine hapa.*
Mkuu wa Mkoa wa mbeya Mhe. Albert Chalamila alisema kuwa, kwa sasa Hospitali Mpya ya Wilaya ya Mbarali ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa majengo yote na hadi kufikia mwezi Januari hospitali hiyo itaanza kutoa baadhi ya huduma.
Kabla ya kutembelea Hospitali Mpya ya Wilaya ya Mbarali, Mhe. Waziri Jaffo siku ya tarehe 14/12/2019 alianza Mkoa wa Dodoma, Mkoa wa Njombe pamoja na Mkoa wa Mbeya, na baadae ataendelea na ratiba zake za mikoa mingine.
Mwisho
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa