Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Moses Nauye leo amefanya ziara katika Mkoa wa Mbeya na kufanya kikao na viongozi mbalimbali wa Mkoa kuhusiana na zoezi la anwani za makazi ambapo ameridhishwa na kasi ya zoezi hilo ambalo bado linaendelea kufanyika.
Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali, Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, madiwa, watendaji wa mitaa na kata. Waziri nape amesema serikali imejipanga kukamilisha zoezi hilo kwa wakati na kwa maeneo ambayo yatakuwa na migogoro wataendele kuyatafutia ufumbuzi ili zoezi hilo liweze kukamilika.
Nape aliambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi (Elimu), Mh David Silinde pamoja na viongozi mbalimbali wanaohusiana Maswala ya anwani za Makazi katika kukagua maendeleo ya zoezi hilo katika Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amemshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya ambapo kwa Mkoa wa Mbeya umeweza kuchangia zaidi ya milioni 300 lakini bado wataangalia jinsi ya kutumia mapato ya ndani ili kuweza kukamilisha zoezi hilo ambalo litaleta alama kubwa katika nchi na kuleta maendeleo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa