Wizara ya fedha leo Ijumaa July21 imetoa semina ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma Mkoani Mbeya juu ya namna ya kutoa Elimu kwa Wananchi wanaowaongoza juu ya Nini maana ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2020 na 2050 na ni Wapi Taifa linaelekea
Seminar hiyo imefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwira kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera imejumuisha watumishi wa Umma, Taasisi binafsi na Viongoizi wa Dini na imefanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Akizungumza baada ya kufungua Kikao hicho Kanali Mwira ameiomba Wizara ya fedha kuwatumia wataalam katika kutathimini uhai wa Dira ya Maendeleo ya Taifa.
Aidha Mwira amesema ni vema Maafisa Mahusiano wakatumia taaluma yao vizuri hasa katika kutengeneza mahusiano mema na mamlaka na Taasisi za kimataifa ili kuichochea Dira hiyo kufanikiwa.
Washiriki wa semina hiyo wamesema elimu waliyoipata wataitumia vyema ingawa wameiomba Wizara kutoishia juu katika utoaji elimu badala yake wawafate Wananchi wa chini ili wawape elimu hiyo kabla ya kwenda kukusanya Maoini.
Alfred Missana Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya fedha amesema moja ya mafanikio ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ni pamoja na nchi ya Tanzania kufika uchumi wa kati wa chini Mwaka 2020
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki MilikiĀ©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa