Uwekezaji Mkoa wa Mbeya
Mkoa wa Mbeya una eneo la kilometa za mraba 35,493 zilizogawanyika katika Wilaya 5 ambazo ni Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya na Rungwe. Mkoa una jumla ya Halmashauri 7 zikiwepo Halmashauri za Wilaya 6 na Halmashauri ya Jiji. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Mkoa wa Mbeya una idadi ya wakazi 1,708,548 ambapo wanaume wapo 818,858 na wanawake 889,690.
Uchumi wa Mkoa unategemea kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, uvunaji mazao ya maliasili, biashara, uzalishaji viwandani na ajira katika taasisi za Serikali na sekta binafsi.
Kilimo kinaajiri asilimia 80 ya watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi na kinachangia asilimia 68 ya Pato la Mkoa kwa mwaka. Shughuli za misitu na uvuvi zinachukua nafasi ya pili baada ya kilimo kwa kuajiri asilimia 6.4 na kufuatiwa na Biashara na viwanda zinazoajiri asilimia 4.9 ya wakazi wote katika Mkoa. Juhudi zinazoendelea katika Mkoa ni kukuza sekta ya viwanda na biashara na kukuza mitaji katika kilimo ili kuweza kuajiri watu wengi zaidi.
Pato la Mkoa limepanda kutoka shilingi trilioni 2.352 mwaka 2008 hadi shilingi trilioni 6.761 mwaka 2015. Wastani wa pato la mtu limeongezeka kutoka shilingi 940,310 mwaka 2008 hadi shilingi 2,301,974 mwaka 2015. Mkoa unachangia asilimia 7.4 ya pato la Taifa ukishika nafasi ya tatu baada ya Dar es Salaam na Mwanza (Ofisi ya Taifa ya Takwimu, 2015).
Uwekezaji katika Mazao Mapya yenye Fursa ya Biashara Nje ya Nchi
Mikutano ya wadau imefanyika na kuweka mikakati ya kuzalisha mazao hususan ya bustani (mboga, maua, matunda na viungo) kwa ajili Masoko ya kimataifa kupitia Uwanja wa Ndege Songwe. Wakulima 285 wamefikiwa na kuhamasishwa kuunda umoja na kutenga maeneo maalum ya kilimo cha kibiashara. Kazi kuandaa na kuimarisha vikundi vya wakulima wa mazao ya bustani inaendelea. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imetenga eneo la ekari 100 kwa ajili ya kujenga maghala ya hifadhi (cold rooms).
Kupitia mradi wa MIVARF maghala baridi (cold rooms) yanatarajiwa kujengwa katika Halmashauri ya Rungwe ambapo taratibu zote za kumpata mkandarasi zimekamilika ili kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao la parachichi kwa kuwa na miundombinu ya kuhifadhi kabla ya kusafirisha mazao katika masoko.
Hali ya Utengaji wa Maeneo ya Uwekezaji katika Mkoa wa Mbeya
Na |
Halmashauri |
Eneo |
Ukubwa (Ha) |
Matumizi |
Hali ya Upimaji |
Hali ya Fidia |
Hali ya Huduma |
1
|
Mbarali DC
|
Rujewa
|
6.67
|
Viwanda
|
Limepimwa
|
Halidaiwi fidia
|
Huduma zote muhimu zipo
|
Madabila
|
16.08
|
Viwanda
|
Limepimwa
|
Linahitaji Fidia
|
Huduma zote muhimu zipo
|
||
Ubaruku
|
75
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Linahitaji Fidia
|
Lipo karibu na Miundombinu Muhimu
|
||
Madabila
|
5.01
|
Viwanda
|
Limepimwa
|
Linahitaji Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Chimala
|
12.04
|
Viwanda
|
Limepimwa
|
Linahitaji Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Igurusi
|
13.48
|
Viwanda
|
Limepimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Madabila
|
27.4
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Lipo Barabara ya Badabila - Mafinga
|
||
Lugelele
|
15.28
|
Kilimo
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Lipo pembezoni mwa TANZAM Road
|
||
103.88
|
Kilimo
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Lipo pembezoni mwa TANZAM Road
|
|||
60.2
|
Kilimo
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Lipo pembezoni mwa TANZAM Road
|
|||
Rujewa (Mogelo)
|
75
|
Kilimo
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Lipo Barbara kuu ya Rujewa- Madabila
|
||
Chimala
|
23.12
|
Kilimo
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Lipo Pembezoni mwa Barabara ya Mbeya-Iringa
|
||
Igurusi
|
25
|
Kilimo
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Barabara ya Mbeya-Iringa
|
||
Jumla
|
458.16
|
|
|||||
2
|
Chunya DC
|
Itewe
|
4.16
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
Mbugani
|
9.01
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Kibaoni
|
2
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Makongorosi
|
5.12
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Kiwanja
|
3
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Sinjili
|
7
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Jumla
|
30.29
|
|
|||||
3
|
Mbeya DC
|
Inyala
|
44
|
Viwanda na Bandari Kavu
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
Tembela (73 ha)
|
138.6
|
Kilimo cha Maua
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Santiliya (23 ha)
|
|||||||
Itunda(30 ha)
|
|||||||
Ilembo (3 ha)
|
|||||||
Iyunga Mapinduzi (6.6 ha)
|
|||||||
Sanje (3ha)
|
|||||||
Tembela (56 ha)
|
89
|
Kilimo cha Pareto
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Itawa (6ha)
|
|||||||
Ilembo (7 ha)
|
|||||||
Maendeleo (8 ha)
|
|||||||
Iyunga Mapinduzi (12ha)
|
|||||||
|
Tembela (57 ha)
|
370
|
Kilimo cha mbogamboga
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
|
Mshewe (142ha)
|
|||||||
Inyala (76 ha)
|
|||||||
Ijombe (43ha)
|
|||||||
Ulenje (13ha)
|
|||||||
Itewe (27 ha)
|
|||||||
Utengule –Usongwe (12ha)
|
|||||||
Ilungu
|
8
|
Kilimo cha Vitunguu Swaumu
|
|
|
|
||
Njenjele
|
10.5
|
Kilimo cha Alizeti
|
Imepimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Ipwizi
|
53
|
Kilimo cha Alizeti
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
|
||
Ileya
|
120
|
Kilimo cha Alizeti
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
|
|
Inyala
|
44
|
Viwanda na Bandari kavu
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
Bonde la Songwe
|
1.6
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Jumla
|
878.7
|
|
|
|
|
||
4
|
Kyela
|
Matema (Ngyekye)
|
493.6
|
Kilimo na Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
Ngonga
|
40
|
Hotel
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Busale
|
11.4
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Kyela mjini
|
47.4
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Jumla
|
|
592.4
|
|
|
|
|
|
5
|
Mbeya CC
|
Nsoho
|
209
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
Mwansekwa
|
65
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Mwansanga
|
140
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Iduda
|
241
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
||
Jumla
|
655
|
|
|||||
6
|
Rungwe DC
|
Vijiji vya Ilima, Katunduru na Lubanda, Kata ya Ilima
|
80
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
|
|
Vijiji vya Ikuti (Kinyika) na Kijiji cha Ibungu, Kata ua Ikuti
|
20
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
|
Kijiji cha Mbeye 1, Ndaga na Ntokela
|
8
|
Viwanda
|
Halijapimwa
|
Halijalipwa Fidia
|
Huduma muhimu zipo karibu
|
|
Jumla
|
108
|
|
|||||
|
Jumla kuu
|
2,722.55
|
|
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa