Mbarali District
Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya tisa na Halmashauri kumi zinazounda Mkoa wa Mbeya. Wilaya hii ilianzishwa mnamo tarehe 7 Julai, 2000 kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kupatiwa cheti kilichosainiwa tarehe 5 June, 2003.
UTANGULIZI.
Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya tisa na Halmashauri kumi zinazounda Mkoa wa Mbeya. Wilaya hii ilianzishwa mnamo tarehe 7 Julai, 2000 kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kupatiwa cheti kilichosainiwa tarehe 5 June, 2003.
MAHALI ILIPO NA MIPAKA YAKE.
Wilaya ya Mbarali ipo kati ya nyuzi 33.40 na 35.40 Longitudo kuelekea upande wa Mashariki, nyuzi 7.41 na 9.25 kusini ya Ikweta. Upande wa Kaskazini Mashariki, inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini, upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Njombe, upande wa Kusini kabisa inapakana na wilaya ya Mbeya na Kaskazini inapakana na Wilaya ya Chunya.
1.2. ENEO NA MATUMIZI YA ARDHI.
Wilaya ina jumla ya eneo la Kilometa za mraba 16,000 na mgawanyo wa matumizi ya ardhi ni kama inavyoonyesha kwenye jedwali No. 1.
JEDWALI I:
NA
|
MATUMIZI YA ARDHI
|
KM ZA
MRABA |
HEKTA
|
ASILIMIA
YA UWIANO |
1
|
Ardhi kwa ajili ya kilimo
|
3,215
|
321,500
|
20.09
|
2
|
Eneo la wanyama pori
|
5,200
|
520,000
|
32.5
|
3
|
Hifadhi ya Misitu
|
172
|
17, 200
|
1.1
|
4
|
Eneo la makazi
|
6,078
|
607,800
|
38.0
|
5
|
Uwanda wa Tambarare, vilima, maeneo oevu na ufugaji
|
2,590
|
259,000
|
16.2
|
|
JUMLA
|
16,000
|
1,600,000
|
108
|
1.3. SURA YA NCHI
Wilaya ya Mbarali ipo uwanda wa chini wa tambarare wenye nyasi na sehemu kubwa ya Wilaya imepitiwa na Bonde la Ufa na maeneo yenye miinuko kwa upande wa Magharibi, ikiwa na mito mitatu ya kudumu. Vile vile Wilaya ina chanzo kikuu cha maji ambacho ni Mto Ruaha Mkuu ambao baadaye huungana na mto Rufiji na kumwaga maji katika Bahari ya Hindi.
Wilaya imegawanyika katika kanda tatu za KIIKOLOJIA ambazo ni Uwanda wa Msangaji, Uwanda wa kati wa Usangu na Tambarare za Kusini mwa Usangu.
JEDWALI II:
NA
|
KANDA
|
MAHALI ILIPO
|
ALTITUDE (M)
|
UDONGO WA MVUA
|
SHUGHULI KUU ZA KIUCHUMI
|
1
|
Uwanda wa Msangaji (kanda ya Kaskazini)
|
Ruaha National Park
|
1200-1800
|
Udongo wa mawe wenye rutuba ndogo
Mvua milimita 500-900 kwa Mwaka Unyevunyevu miezi 3-5 |
Eneo lipo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA)
|
2
|
Uwanda wa kati wa tambarare ya Usangu (Ukanda mkuu wa ufugaji)
|
Ruiwa
Ut/Usangu Rujewa Mapogoro Sehemu ya kata ya Mawindi |
1000-1400
|
Udongo mweusi na kichanga
Mvua mm 450-650 kwa mwaka Unyevunyevu miezi 3-4 |
Kilimo cha mazao ya:
Mtama Uwele Ufugaji Mahindi Mpunga |
3
|
Tambarare za Kusini Usangu (ukanda wa kusini – kanda ya kilimo)
|
Ilongo
Rujewa Chimala Mapogoro Igurusi Ubaruku |
750-1000
|
Mvua haba mm 360-750
|
Kilimo cha mazao ya:
Mahindi Karanga Pamba Kilimo cha umwagiliaji Mpunga Ufugaji |
1.4. HALI YA HEWA NA UOTO
Wilaya ya Mbarali ipo katika latitude inayoanzia mita 1,000 – 1,800 juu ya usawa wa Bahari. Wastani wa joto ni kati ya nyuzi 25c na 30c. Wastani wa mvua hutofautiana kati ya milimita 300-940, hata hivyo kuna misimu miwili yaani msimu wa kiangazi ambao huanzia mwezi Mei – Novemba na msimu wa mvua ambao huanza Desemba – Aprili
Kwa ujumla Wilaya yote iko ndani ya uwanda wa Tambarare katika Bonde la Usangu ambalo lina uoto wa Asili aina ya Mipogoro.
Hali ya Mvua kwa Miaka Mitano iliyopita ni kama ifuatavyo:
NA
|
MWAKA
|
WASTANI WA MVUA (MM)
|
1
|
2005/2006
|
300.00
|
2
|
2006/2007
|
800.00
|
3
|
2007/2008
|
450.00
|
4
|
2008/2009
|
400.00
|
5
|
2009/2010
|
412.80
|
6
|
2010/2011
|
428.00
|
7
|
2011/2012
|
473.96
|
8
|
2012/2013
|
216.48
|
9
|
2013/2014
|
770
|
Hali hii ya upunguaji wa Mvua, inaathiri sana uzalishaji wa mazao ya kilimo hususani mpunga ambao ndio tegemeo kuu la mapato yetu ya ndani.
1.5. MUUNDO WA UTAWALA NA MAKABILA.
Muundo na utawala wa Wilaya ya Mbarali ni kama inavyoonyesha kwenye jedwali.
JEDWALI III
TARAFA
|
MAJIMBO YA UCHAGUZI
|
KATA
|
VIJIJI
|
VITO NGOJI
|
KAYA
|
WAH. MADIWANI
|
||
KUCHAGU
LIWA |
KUTEULIWA
|
JML
|
||||||
2
|
1
|
20
|
103
|
713
|
69,888
|
|
|
|
1.6 MAKABILA
Makabila makuu yaliyopo Wilayani Mbarali ni Wasangu, Wahehe, Wakinga, Wabena na Wanyakyusa. Vile vile yapo makundi madogo ya makabila wakiwemo Wasukuma, Wanji, Wabarbeig na Wagogo.
Makundi mengi ya makabila haya ni wakulima na wafugaji ambao walihamia bonde la Usangu kutoka Mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma.
1.7. IDADI YA WATU
Kufuatia sensa ya kitaifa ya idadi ya watu ya mwaka 2012, Wilaya ya Mbarali sasa ina jumla ya watu 300,517 ambao kati yao 145,867ni wanaume na 154,650 ni wanawake ikiwa na ukuaji wa 2.8%.
1.8. IDADI YA WATUMISHI.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ina jumla ya watumishi 2,527. Mahitaji ni watumishi 2,971 hivyo kuna upungufu wa watumishi wapatao 1,012 kama jedwali linavyoonyesha hapa chini;
JEDWALI IV
Na
|
IDARA/KITENGO
|
IKAMA ILIYOIDHINI SHWA
|
WATUMISHI WALIOPO
|
UPU NGUFU
|
ZIADA
|
1
|
Utawala na Utumishi
|
144
|
130
|
14
|
-
|
2
|
Fedha na Biashara
|
22
|
19
|
3
|
-
|
3
|
Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
|
6
|
5
|
1
|
-
|
4
|
Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
|
134
|
83
|
51
|
-
|
5
|
Mifugo na Uvuvi
|
128
|
48
|
80
|
-
|
6
|
Elimu ya Msingi
|
1648
|
1193
|
455
|
-
|
7
|
Elimu ya Sekondari
|
495
|
434
|
61
|
-
|
8
|
Maji
|
13
|
7
|
6
|
-
|
9
|
Ujenzi
|
30
|
21
|
9
|
-
|
10
|
Afya
|
688
|
365
|
323
|
-
|
11
|
Ardhi na Maliasili
|
26
|
21
|
5
|
-
|
12
|
Maendeleo ya Jamii
|
27
|
23
|
4
|
-
|
|
JUMLA
|
2,971
|
2,527
|
1,012
|
-
|
1.9: MWENENDO WA MAPATO NDANI YA HALMASHAURI
Halmashauri imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii kupitia Mapato yake ya Ndani yanayotokana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushuru wa mazao, ushuru kutokana na huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri. Mwenendo wa mapato ya ndani ya Halmashauri ni kama ifuatavyo:-
JEDWALI V
NA
|
MWAKA
|
MAKISIO
|
MAPATO
|
ASILIMIA (%)
|
1
|
2007/2008
|
319,882,060
|
487,449,295
|
152
|
2
|
2010/2011
|
478,894,538
|
666,742,372
|
139
|
3
|
2009/2010
|
721,124,000
|
639,527,000
|
88.7
|
4
|
2010/2011
|
728,757,700
|
621,890,570
|
85.3
|
5
|
2011/2012
|
773,027,000
|
934,388,639
|
121
|
6
|
2012/2013
|
1,348,748,000
|
915,496,546
|
67.9
|
7
|
2013/2014
|
1,602,798,000
|
1,396,807,050.55
|
87.1
|
8
|
2014/2015
|
2,672,063,706
|
1,921,741,556.72
|
72
|
|
|
|
|
|
2.0: SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
Uchumi wa Wilaya ya Mbarali unategemea kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa mali vijijini hasa sekta ya Kilimo, wastani wa asilimia 83 ya wakazi Wilaya ya Mbarali hujishughulisha na kilimo, shughuli zingine za kiuchumi ni pamoja na ufugaji, uvuvi na biashara ndogondogo; kwa ujumla wake pato la mkazi wa Mbarali ni shilingi 376,500/= kwa mwaka.
2.1 KILIMO
Asilimia 83 ya wakazi wa Wilaya ya Mbarali hujishughulisha na kilimo na ufugaji. Mazao muhimu ya chakula ni pamoja na Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu, Mihogo, Maharage na Mtama. Hata hivyo mpunga huzalishwa kama zao la chakula na biashara. Mazao ya biashara ni Alizeti, Karanga na Mazao ya bustani.
Kutokana na hali ya hewa isiyotabirika na kupungua kwa mvua, Halmashauri imekuwa inawekeza katika Kilimo cha umwagiliaji.
Mpaka sasa, Wilaya ya Mbarali ina jumla ya skimu za umwagiliaji 80 zenye jumla ya hekta 78,953. Kati ya hizo skimu 34 zimeboreshwa zenye jumla ya eneo linalofaa kulimwa hekta 41,724 lakini zinazolimwa ni 23,519. Aidha skimu 46 hazijaboreshwa zengye jumla ya eneo linalofaa kulimwa hekta 37,229 lakini zinazolimwa ni 20,989.
Juhudi zinaendelea za kuboresha miundombinu ya skimu za kilimo cha umwagiliaji, kuwajengea uwezo wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija zaidi, Ujenzi wa miundombinu ya masoko (maghala na viwanda vya usindikaji) na kuboresha barabara za vijijini zipitike kwa urahisi.
2.2. MALIASILI
Wilaya ina utajiri wa maliasili mbalimbali ikiwa ni pamoja na misitu, wanyamapori, madini, ufugaji nyuki, samaki na sehemu ya hifadhi ya Taifa Ruaha, vilevile pori la akiba la Usangu.
3.0 HUDUMA ZA KIJAMII NA FURSA ZILIZOPO
3.1 ELIMU
Wilaya ina shule/vyuo kama ifuatavyo:
Jedwali vII
NA
|
AINA YA SHULE
|
SERIKALI
|
BINAFSI
|
TAASISI
|
JUMLA
|
1
|
Shule za awali
|
100
|
-
|
2
|
102
|
2
|
Shule za msingi
|
103
|
2
|
-
|
105
|
3
|
Shule za sekondari
|
16
|
1
|
6
|
23
|
4
|
Vituo vya EWW
|
5
|
-
|
-
|
5
|
5
|
Vituo vya MUKEJA
|
12
|
-
|
-
|
12
|
Idadi ya wanafunzi wa shule za msingi 51,999
Idadi ya wanafunzi wa shule za sekondari 9,580
Idadi ya walimu shule za msingi 1,193
Uwiano wa walimu na wanafunzi 1:44
Kwa Mwaka wa masomo 2013 kiwango cha ufaulu kwa Elimu ya Msingi ni 70.0%
Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuingia Sekondari ni 4143. Wanafunzi hao wote walipata nafasi ya kujiunga na Kidato cha Kwanza.
Kiwango cha ufaulu Kwa Elimu ya Sekondari ni; Kidato cha pili 94.87% na Kidato cha nne 71.23% (83.23%).
Aidha kwa upande wa Walimu hali halisi iko kama ifuatavyo:
JEDWALI VII
Sekta
|
Idadi ya Walimu
|
Asilimia ya Upungufu
|
||
Wanaohitajika
|
Waliopo
|
Upungufu
|
||
Elimu ya Msingi
|
1299
|
1193
|
106
|
8
|
Elimu ya Sekondari
|
597
|
506
|
91
|
15
|
3.2 AFYA
Wilaya ina vituo vya kutolea huduma ya afya kama ifuatavyo:
JEDWALI VIII
NA
|
VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
|
SERIKALI
|
BINAFSI
|
TAASISI
|
JUMLA
|
1
|
Hospitali
|
1
|
-
|
1
|
2
|
2
|
Kituo cha afya
|
5
|
-
|
1
|
6
|
3
|
Zahanati
|
34
|
2
|
4
|
40
|
Kwa upande wa Rasilimali watu katika Idara ya Afya, hali iko kama ifuatavyo:
Shule
|
Idadi ya Watumishi
|
Asilimia ya Upungufu
|
||
Wanaohitajika
|
Waliopo
|
Upungufu
|
||
Hospitali ya Wilaya
|
211
|
164
|
47
|
22.3
|
Afya Kinga
|
26
|
11
|
15
|
57.7
|
Vituo vya Afya 5
|
195
|
87
|
108
|
55.4
|
Zahanati 34
|
510
|
185
|
325
|
63.7
|
JUMLA
|
942
|
447
|
495
|
52.5
|
3.3 MAJI
Wilaya ya Mbarali ina mtiririko wa mito inayoanzia safu ya milima ya kipengele na uproot, vyanzo hivi vimekuwa mtego wa maji ya bomba kwa vijiji 76 kati ya 93 vya Wilaya nzima.
JEDWALI VI:
NA
|
VYANZO VYA MAJI
|
IDADI
|
IDADI YA VIJIJI VINAVYONUFAIKA NA HUDUMA
|
IDADI YA WATU WANAONUFAIKA NA HUDUMA
|
1
|
Miradi ya kutegwa (gravity scheme)
|
10
|
52
|
160,848
|
2
|
Visima virefu (Borehole)
|
36
|
15
|
36,104
|
3
|
Visima vifupi (Borehole)
|
47
|
10
|
13,533
|
|
JUMLA
|
93
|
77
|
210,485
|
3.4 BARABARA
Wilaya ina mtandao wa barabara zilizoanzishwa zenye urefu wa km 1,308.2 ambazo kati ya hizo, barabara zenye urefu wa km 305.5 zinahudumiwa na meneja wa TANROADS na km 1002.7 zinahudumiwa na Halmashauri. Barabara zinazohudumiwa na Halmashauri zimegawanyika kama ifuatavyo;
JEDWALI VII
NA
|
AINA YA BARABARA
|
UREFU
|
1
|
Barabara ya changarawe
|
Km 216.15
|
2
|
Barabara ya changarawe/udongo
|
Km 786.55
|
Aidha kuna km 555.95 ambazo hazijaandikishwa na zinahudumiwa na Halmashauri, baada ya kupitishwa na Baraza la Madiwani mwaka 1998 ili kuweza kufikia maeneo ya uzalishaji na utawala, ili kuboresha ujenzi wa uchumi katika Wilaya. Kati ya km 555.95 km 86.7 ni za changarawe na km 469.25 ni za udongo.
3.5 VYAMA VYA USHIRIKA
Vyama vya ushirika ni vyombo muhimu katika kumkomboa mwananchi kutokana na umaskini. Hali ya vyama vya ushirika katika wilaya ya Mbarali ni kama ifuatavyo:
JEDWALI VIII
NA
|
AINA YA USHIRIKA
|
WANACHAMA
|
MTAJI
Tshs.’000,000 |
MIKOPO Tshs.’000’000
|
||||||
IDADI
|
MOJA
MOJA |
VIKUNDI
|
JUMLA
|
HISA
|
AMANA
|
AKIBA
|
TOLE
WA |
REJESHA
|
||
1
|
Ushirika wa Akiba na Mikopo
|
24
|
7,191
|
209
|
7,400
|
1282.5
|
430.9
|
2028.8
|
23.404.7
|
14,347.3
|
2
|
Ushirika wa usafirishaji wa mazao ya kilimo
|
3
|
86
|
-
|
86
|
12.4
|
-
|
-
|
-
|
-
|
3
|
Ushirika wa kilimo na masoko
|
8
|
4,168
|
14
|
4,182
|
316.6
|
-
|
-
|
-
|
-
|
4
|
Ushirika wa wafugaji
|
1
|
18
|
-
|
18
|
0.64
|
-
|
-
|
-
|
-
|
5
|
Ushirika wa kilimo na umwagiliaji
|
9
|
2,808
|
8
|
2,816
|
12.3
|
-
|
-
|
-
|
-
|
6
|
Ushirika wa biashara ya samaki
|
4
|
170
|
0
|
170
|
13.85
|
-
|
-
|
-
|
-
|
7
|
Wabeba mifugo
|
1
|
19
|
|
|
1
|
|
|
|
|
|
JUMLA
|
50
|
15397
|
2028
|
15705
|
2593
|
378
|
2581
|
15801
|
12318
|
3.6. VIKUNDI VYA KIUCHUMI VYA WANAWAKE NA VIJANA
Katika kuhakikisha umaskini unapungua kwa jamii wa wilaya ya Mbarali huduma ya mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake na vijana imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1998 hadi 2013 kama inavyoonyesha:-
JEDWALI IX:
MWAKA
|
VIKUNDI
|
MKOPO TOLEWA
|
RIBA (10%)
|
MKOPO + RIBA
|
MAREJESHO
|
BAKI
|
% YA MAREJESHO
|
Bakaa 2006
|
82
|
70,993,000
|
9,122,800
|
80,115,800
|
79,626,554
|
1,233,454
|
99.39
|
2007
|
17
|
18,000,000
|
1,800,000
|
19,800,000
|
19,590,000
|
210,000
|
98.93
|
2008
|
14
|
15,200,000
|
1,520,000
|
16,720,000
|
16,180,000
|
540,000
|
96.77
|
2009
|
4
|
4,000,000
|
400,000
|
4,400,000
|
4,400,000
|
0
|
100
|
2010
|
12
|
10,350,000
|
1,755,000
|
11,385,000
|
11,385,000
|
0
|
100
|
2013
|
3
|
6,000,000
|
600,000
|
6,600,000
|
4,600,000
|
2,000,000
|
69.69
|
JUMLA
|
32
|
124,543,000
|
15,197,800
|
139,020,800
|
135,781,554
|
3.983,454
|
97.66 |
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa