SEKSHENI YA ELIMU
Seksheni hii ina lengo la kusaidia au kuwezesha utoaji huduma za uendelezaji wa Elimu ikijumuisha usimamizi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na inayotolewa katika njia isiyo rasmi; na mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Huduma za Elimu
•Kuratibu uongozi wa shule za awali, Msingi, Sekondari, elimu ya watu wazima na Elimu rasmi
•Kuratibu ajira na usambazaji wa walimu wa shule za awali, msingi na sekondari katika Mkoa
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Elimu na mafunzo ya ufundi ndani ya Mkoa na kutoa Ushauri kadiri inavyohitajika.
•Kusimamia mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu katika Mkoa.
•Kuratibu ukusanyaji, tathimini, uunganishaji/uandaaji, kutafsiri na kutoa taarifa/takwimu za elimu na mafunzo ya ufundi katika Mkoa
•Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa taarifa za ukaguzi
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya utekelezaji wa sera ya utamaduni na michezo
•Kuratibu shughuli zinazohusiana na michezo katika Mkoa na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Mkoani.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa