Kikao Cha kwanza Cha Maandalizi Maonyesho ya Sherehe za Wakulima Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kimeketi Leo April 29/2025 katika Ukumbi wa Mkoa na Kujadili Namna Bora ya Kuanza michakato wa Maandalizi ya Sherehe hizo ambazo Kila Mwaka hufanyika kuanzia Tarehe 01-08.
M/kit wa Kamati ya Maandalizi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Makongoro Nyerere amefungua Kikao hicho kwa kuwapongeza wajumbe kwa muitikio wao wa siku ya kwanza na kuwataka kuwa wamoja, kutochoka katika Kila hatua itakayofanywa ya maandalizi Lengo ikiwa ni kufanya Vizuri zaidi Mwaka huu.
Katibu wa sekretarieti ya maandalizi ya sherehe za maonyesho ya wakulima 88 Kanda ya nyanda za juu kusini Saidi Madito amesema tayari maandalizi yameshaanza hivyo anaomba taasisi mbalimbali zimehamasike na kujitokeza kusapoti Sherehe hizi ili Mwaka huu ziwe na ubora zaidi.
Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Rodrck Lazaro Mpogolo amewatoa shaka Wajumbe wa Kikao kuwa Maboresho ya uwanja wa maonyesho ya wakulima Nane Nane wa John Mwakangale ambao Serikali iliagiza ufanyiwe Ukarabati, Licha ya Kwamba haujakamilika lakini haitakuwa sababu ya Sherehe hizo kutofanyika.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa