Mkoa wa Mbeya una jumla ya mifugo 3,095,116 kati ya hiyo idadi ya ng’ombe ni 653,304; mbuzi ni 195,569 na kondoo ni 79,850. Mchanganuo wa idadi ya mifugo ni kama inavyooneshwa katika jedwali Na. 3.4.1
Jedwali Idadi ya Mifugo kwa aina Kiwilaya hadi Juni, 2017
Mnyama
|
Halmashauri
|
Jumla
|
||||||
Busokelo
|
Chunya
|
Mbarali
|
Mbeya (J)
|
Mbeya
|
Kyela
|
Rungwe
|
||
Ng’ombe (asili)
|
23,847 |
201,819 |
168,580 |
5,355 |
72,341 |
42,963 |
59,022 |
573,927 |
Ng’ombe (kisasa)
|
12,641 |
307 |
2,524 |
3,820 |
7,079 |
2,785 |
30,221 |
59,377 |
Mbuzi (asili)
|
9,826 |
33,879 |
85,924 |
4,472 |
33,155 |
4,869 |
21,123 |
193,248 |
Mbuzi(kisasa)
|
136 |
54 |
71 |
570 |
888 |
0 |
602 |
2,321 |
Kondoo
|
4,954 |
10,251 |
40,993 |
673 |
5,698 |
1,369 |
15,912 |
79,850 |
Nguruwe
|
21,982 |
1,646 |
12,843 |
5,096 |
21,646 |
32,887 |
55,213 |
151,313 |
Kuku (asili)
|
254,376 |
142,087 |
242,651 |
60,151 |
327,322 |
352,690 |
554,345 |
1,933,622 |
Kuku (kisasa)
|
8,932 |
0 |
4,273 |
70,323 |
15,000 |
0 |
2,930 |
101,458 |
JUMLA |
3,095,116 |
Chanzo: Halmashauri za Wilaya na Halmashauri ya Jiji 2016
Mazao ya Mifugo
Mazao makuu ya mifugo yanayozalishwa ni nyama, maziwa, mayai na ngozi. Maziwa yanazalishwa kupitia wafugaji moja moja na mitandao ya ufugaji kiwilaya ukiwemo Mtandao wa wafugaji Rungwe wenye vikundi 32, MVIWAWIMBE (Halmashauri ya Mbeya) vikundi 15 na MVIWAMA (Jiji la Mbeya) wenye vikundi 11. Kuna viwanda vidogo vya kusindika maziwa ambavyo ni Mbeya Milk, Isanga Dairy Cooperative Society na MATI – Uyole vya Jijini Mbeya. Wadau wengine ni Mwasa Dairies na Faraja Group waliopo Wilayani Rungwe. Mwaka 2016/2017 lita 139,325,929 za maziwa yenye thamani ya shillingi 111,460,743,200 yalizalishwa. Aidha, Mwaka 2016/17 vipande vya ngozi 46,204 vya ng’ombe, mbuzi 31,004 na vipande 4,584 vya ngozi ya kondoo vyenye thamani ya jumla ya shilingi 231,545,600 vilikusanywa na kuuzwa ndani na nje ya nchi.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mkoa wa Mbeya unajitosheleza katika kuzalisha nyama na kiasi kikubwa cha mifugo huuzwa nje ya Mkoa. Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kilo 15,549,136 za nyama zilizalishwa zenye thamani ya shilingi 93,294,816,000.
Mkoa kwa mwaka 2016/2017 umekusanya maduhuli yenye thamani ya 36,895,750,000 baada ya kusafirisha ng’ombe 56,624 na wanyama wengine (Small Stock) 34,427. Pia Mkoa una machinjio kubwa 33 na makaro 85 ambayo yamejengwa na kukarabatiwa kupitia miradi ya DADPs na Mpango wa Kuendeleza Ngozi Tanzania. Mkoa una majosho 77 yanayotumika. Kuna vituo 29 vya kutolea huduma za mifugo (VHS) kati ya hivyo 10 vimesajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania. Aidha, Mkoa una jumla ya maduka 720 ya kuuzia nyama.
Katika kuepusha migororo ya wakulima na wafugaji, Mkoa kwa kupitia Halmashauri umeweza kutenga ekari 1,024,517 kwa ajili ya malisho hasa katika Halmashauri za wilaya za Chunya, Mbarali na Mbeya. Kuna shamba la kuzalisha mbegu za malisho la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi eneo la Langwila Wilayani Mbarali lenye ukubwa wa hekta 294. Shamba hili linatarajiwa kuzalisha mbegu za malisho kwa ajili ya mashamba darasa ya malisho na mashamba ya malisho ya taasisi na watu binafsi. Pia Kituo cha Utafiti wa Mifugo – Uyole huzalisha na kusambaza mbegu aina ya Rhodes Boma, miti malisho na majani makavu (Hay) kwa ajili kituo na wafugaji.
Katika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Makamu wa Rais la kutambua na kusajili mifugo nchini,Mkoa kupitia Halmashauri umekamilisha kazi ya kuwatambua na kuasajili wafugaji na mifugo. Kazi ya kupiga chapa na kuweka heleni ng’ombe wa asili 573,927 na wa maziwa 59,377 umezinduliwa rasmi na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa katika Halmashauri za Chunya tarehe 11.07.2017 na Mbarali tarehe 14.07.2017. Zoezi la kupiga chapa na kuweka heleni linatajia kukamilika ifikapo tarehe 31.07.2017
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa