Mkoa unapata mvua kwa kiwango cha mm 600 katika maeneo ya Chunya na mm 2800 katika maeneo ya Rungwe, kwa mwaka. Vyanzo vikuu vya maji kwa jamii kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ni mito, chemichemi na visima. Aidha, Mkoa una Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira 7 mijini na; Kamati za maji 368 na COWSO 81 vijijini. Mwaka 2015 huduma ya maji vijijini ilikuwa asilimia 59.2 na hadi Desemba 30, 2017 imefikia asilimia 63.1; na katika miji ya Wilaya na miji midogo, imefikia asilimia 59.5. Miji ya Wilaya na miji midogo ina mtandao wa maji wenye urefu wa kilomita 301.4. Aidha, hadi Desemba 30, 2017, huduma ya maji Jijini Mbeya imefikia asilimia 86.9 na, mtandao wa majisafi wenye urefu wa kilomita 748.5 umeenea kwa asilimia 97.3 na mtandao wa majitaka wenye urefu wa kilomita 124.5 umeenea kwa asilimia 14.3. Kwa kuzingatia Sera ya Maji ya Mwaka 2002, Mamlaka za Maji Mkoani Mbeya zinatoa huduma ya majisafi bure kwa jumla ya familia zisizojiweza 269 (familia 142 katika miji ya Wilaya na familia 127 Jijini Mbeya).
Hadi kufikia Desemba, 2017 huduma ya maji safi na salama vijijni imefikia asilimia 63.02 ya wakazi wote waishio vijijini kupitia miradi ya maji yenye vituo vya kuchotea maji vinavyofanyakazi 3,017 kati ya vituo 4,787 iliyopo. Mkoa una Kamati za maji 368 na COWSO 81 vijijini zenye jumla ya shilingi milioni 158.24 (hadi Desemba 30, 2017). Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kila Wilaya kwa maeneo ya vijijini ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 1.
Jendwali Na. 01: Hali ya Huduma ya maji kwa kila Halmashauri
Na |
Halmashauri |
Idadi ya Watu Vijijini |
Idadi ya Watu Wanaopata maji vijijini |
Idadi ya vituo vya kuchotea maji vinavyofanya kazi |
Asilimia ya watu wanaopata huduma ya Maji (%) |
1 |
Busokelo DC
|
96,348 |
77,689 |
322 |
80.6 |
2 |
Chunya DC
|
141,794 |
50,542 |
104 |
35.6 |
3 |
Kyela DC
|
191,536 |
132,000 |
528 |
68.92 |
4 |
Mbarali DC
|
300,517 |
210,250 |
841 |
69.96 |
5 |
Mbeya Jiji (PerUrban)
|
138,066 |
103,396 |
148 |
75.00 |
6 |
Mbeya DC
|
244,021 |
125,750 |
503 |
51.53 |
7 |
Rungwe DC
|
240,250 |
142,750 |
571 |
59.42 |
|
Jumla
|
1,352,532 |
842,377 |
3,017 |
63.02 |
Katika hatua za awali za utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), utekelezaji ulianza na miradi midogo midogo inayoleta matokeo ya haraka. Miradi hiyo ilitekelezwa katika miaka ya 2007/2008 na 2008/2009. Fedha za kutekeleza miradi hiyo zilisitishwa kutolewa mwezi Juni, 2009 ili kuanza kutekeleza miradi mikubwa (kwa jina maalufu la vijiji 10 kwa kila Halmashauri) Awamu ya Kwanza WSDP-I, ilianza na miradi 45 katika vijiji 64 kati ya vijiji 83 vilivyoonesha utayari na kuwasilisha maombi ya mradi. Awamu WSDP-I, iliyoishia Juni, 2017 ilijenga jumla ya miradi 29 katika vijiji 36. Aidha, Awamu ya pili, WDDP-II, inaendelea na ujenzi wa miradi 16 iliyobaki katika awamu ya kwanza, katika vijiji 28, ikiwemo miradi ya Luduga-Mawindi (Mbarali) na Kapapa (Kyela). Aidha, miradi mingine 5 ya Masoko/Mwakaleli na mradi mdogo mmoja wa Busokelo umeongezwa katika awamu –II na kufanya jumla ya miradi 23. Hivyo jumla ya miradi iliyokamilika kujengwa hadi kufikia Februri 2017, ni 6 (Iziwa na Itagano, Mbeya Jiji; Lugombo, Simike na Nkunga, Rungwe; na Ilamba, Busokelo) na mingine inaendelea kujengwa, iko wastani wa asilimia 80 ya ujenzi. Aidha, jumla ya fedha zilizopokelewa mwaka wa fedha 2017/018 ni Shilingi 2.33 bilioni, zikujumuisha kulipa madeni ya nyuma; tafadhali rejea kiambatanisho A.
Upanuzi wa Miradi ya Maji katika miji ya Wilaya
Mkoa unakarabati na kupanua jumla ya miradi 6 katika kuboresha miundombinu ya maji katika miji na miji midogo ya Wilaya, kazi hii imeanza kutekelezwa. Jumla ya wakandarasi 6 walipatikana mwishoni mwa Mei 2017. Hadi Desemba 30, 2017, visima virefu sita (kati ya kina cha mita 150 na 80) vimechimbwa Chunya, Kasumulu (Kyela) na Rujewa (Mbarali) kati ya visima 5 vilivyolengwa kuchimbwa. Shughuli nyingine zinazoendelea kufanyika ni ujenzi na upanuzi wa vyanzo vya maji 4, matenki makubwa 4 yenye ujazo wa mita 1015, upanuzi na ukarabati wa bomba zenye urefu wa kilomita 50.5, ununuzi na ufugaji wa pampu 8, solar 2 na mita za maji 2,617; ujenzi wa chujio la maji, nyumba za pampu 5 na Ofisi 1. Kandarasi zote 6 zinagharimu jumla ya Sh. Bilioni 2.94 na kukamilika kwake kutawezesha huduma ya maji mijini kuongezeka kwa 10.5% na kufikia 70.6% ifikapo Juni 2018.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa