Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amewahimiza Wananchi wote(Wanawake) wa Mkoa wa Mbeya na Mikoa Jirani kujitokeza kupata tiba bure ya ugonjwa wa Fistula ya Uzazi na kuchanika msamba kwa wanawake inayotolewa na hospitali ya Rufaa ya wazazi Kanda Mbeya.
Mbali na Matibabu hayo Dkt. Homera amewaalika kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya Fistula duniani ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Mbeya tarehe 23 Mei, 2025 katika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya Kitengo Cha Wazazi (META).
Pia alisisitiza kuwa matibabu haya yanayotolewa ni huduma endelevu ambayo inatolewa (Haina ukomo) na inatolewa bure kabisa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa