Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya tano na Halmashauri saba zinazounda Mkoa wa Mbeya. Wilaya hii ilianzishwa mnamo tarehe 7 Julai, 2000 kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kupatiwa cheti kilichosainiwa tarehe 5 June, 2003.
Wilaya ya Mbarali ipo kati ya nyuzi 33.40 na 35.40 Longitudo kuelekea upande wa Mashariki, nyuzi 7.41 na 9.25 kusini ya Ikweta. Upande wa Kaskazini Mashariki, inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini, upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Njombe, upande wa Kusini kabisa inapakana na wilaya ya Mbeya na Kaskazini inapakana na Wilaya ya Chunya.
Wilaya ina jumla ya eneo la Kilometa za mraba 16,000
Wilaya ya Mbarali ipo katika latitude inayoanzia mita 1,000 – 1,800 juu ya usawa wa Bahari. Wastani wa joto ni kati ya nyuzi 25c na 30c. Wastani wa mvua hutofautiana kati ya milimita 300-940, hata hivyo kuna misimu miwili yaani msimu wa kiangazi ambao huanzia mwezi Mei – Novemba na msimu wa mvua ambao huanza Desemba – Aprili
Makabila makuu yaliyopo Wilayani Mbarali ni Wasangu, Wahehe, Wakinga, Wabena na Wanyakyusa. Vile vile yapo makundi madogo ya makabila wakiwemo Wasukuma, Wanji, Wabarbeig na Wagogo.
Makundi mengi ya makabila haya ni wakulima na wafugaji ambao walihamia bonde la Usangu kutoka Mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma.
Kufuatia sensa ya kitaifa ya idadi ya watu ya mwaka 2012, Wilaya ya Mbarali sasa ina jumla ya watu 300,517 ambao kati yao 145,867ni wanaume na 154,650 ni wanawake ikiwa na ukuaji wa 2.8%.
MKUU WA WILAYA
Mhe. Reuben Mfune
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa