Mkoa wa Mbeya una Halmashauri saba (7) ambazo ni Mbarali, Mbeya DC, Chunya, Kyela, Rungwe, Busokelo na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Halmashauri za Wilaya zinaongozwa na Wenyeviti na Halmashauri ya Jiji inaongozwa na Mstahiki Meya ambao ni Wenyeviti wa Halmashauri, kwa kushirikiana na Wakurugenzi ambao ni Watendaji wakuu wa Halmashauri husika .
Halmashauri za Wilaya za Mkoa waMbeya pamoja na Halmashauri ya Jiji hutoa huduma za Kiuchumi zikiwepo kilimo, mifugo, misitu, Uvuvi, Miundombinu, huduma za jamii kama afya, maji, elimu, maeneo ya burudani, mazishi, mipango miji, kutunza mazingira, ustawi wa jamii, ushirika na mambo mengine yanayoihusu jamii na Taifa kwa ujumla.
Utawala Bora
Utawala bora ni suala linalotekelezwa na Halmashauri zote katika nyanja za:
• Demokrasia
• Ushirikishwaji
• Utawala wa sheria
• Uadilifuwa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
• Uwazi na Uwajibikaji
• Ufanisi katika utendaji kazi
• Mchakato wa kijinsia
• Upangaji mipango
• Ujuziwa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo
• Utekelezajiwa Mipango.
MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.
Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa nasheria hiyo ni kama ifuatavyo:-
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa