Jesdwali Na.1: Mifumo ya Uzalishaji Kilimo (Farming Systems zones)
Na
|
Mfumo wa Kilimo
|
Halmashauri
|
1
|
Migomba - Kahawa
|
Rungwe, Busokelo
|
2
|
Mahindi - Maharage
|
Mbeya rural
|
4
|
Mahindi – Viazi Mviringo
|
Mbeya rural, Rungwe, Busokelo
|
5
|
Tumbaku - Ufugaji
|
Chunya
|
6
|
Mpunga - Ufugaji
|
Mbarali, Kyela
|
7
|
Mahindi Ufugaji
|
Chunya
|
8
|
Mpunga - Kakao
|
Kyela, Rungwe, Busokelo
|
9
|
Mahindi - Ufuta
|
Chunya
|
10
|
Kilimo Mjini (Mahindi, maharage, viazi, ngano, njegere, mboga mboga, ufugaji, biashara na ujasiriamali)
|
Mbeya Jiji
|
Chanzo: ARI Uyole, 2012
1.2 Hali ya mvua
Mvua hutegemewa kunyesha kati mwezi Oktoba na Mei kwa kiwango cha kati ya milimita 650 mm kwa mwaka katika ukanda wa chini na milimita 2,600 kwa mwaka katika Ukanda wa Juu. Kwa msimu wa 2015/2016, mvua zilianza kunyesha katikati ya mwezi Novemba ikilinganishwa na msimu wa 2014/2015 ambapo mvua zilianza kunyesha mwezi Oktoba. Mkoa umepata mvua za wastani katika Wilaya zote na baadhi ya maeneo ya Wilaya za Chunya, Mbarali na Kyela yamepata mvua za wastani na chini ya wastani.
1.3 Uzalishaji wa Mazao ya Kilimo
Uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa 2015/2016 ulifikia tani 3,627,191 , mahitaji ya chakula katika Mkoa ni tani 609,210, hivyo kulikuwa na ziada ya tani 3,017,981. Lengo kwa mwaka 2016/2017 ni kulima hekta 556,374 na kuzalisha tani 4,053,708.
Hali ya Mazao Mashambani
Hali ya mazao mashambani na uvunaji kwa baadhi ya mazao makuu katika Kanda mbalimbali ni kama ifuatavyo:-
Katika Wilaya za Mbeya, Rungwe baadhi ya mahindi yapo katika hatua ya ukuaji na maeneo mengine ya Mkoa mahindi yanaendelea kupandwa kutokana kuchelewa kuanza kwa mvua.
Maharage yaliyopandwa mwezi Novemba katika baadhi ya maeneo yameendelea kukua. Hali ya mazao yaliyopandwa kuanzia mwezi Novemba ni nzuri huku huduma za kupalilia na udhibiti wa visumbufu vya mazao unaendelea vizuri.
Uvunaji wa njegere unaendelea katika maeneo mengi ya Mkoa, na upatikanaji wake sokoni ni wa kuridhisha.
Uvunaji wa viazi unaendelea katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Mbeya na Rungwe kwa viazi ambavyo vilipandwa mwezi Septemba, 2016. Mazao yaliyopandwa kuanzia Desemba 2016 yanaendelea vizuri.
Zao hili lipo katika hatua ya ukuaji na katika maeneo mengine ya mkoa bado wakulima wanapanda.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa